Alhamisi, Aprili 10, 2014

NIMECHEKA SANA LEO NILIPOISOMA HII, HEBU NAWE SOMA UCHEKE WAKATI HUU

Hii story ilinifanya nikatabasamu sababu ni ukweli mtupu.
Kuna jamaa alienda kwa docta sababu alikuwa anaumwa na ugonjwa wa mapafu uliosababishwa na sigara. Maongezi yalikuwa hivi
Docta; "umeanza kuvuta sigara kwa muda gani sasa"
Mgonjwa; "dah miaka kama kumi hivi" docta akapiga hesabu halafu akasema
Docta; "kama ungekuwa huvuti sigara na kuhifadhi hizo hela bank kwa sasa ungekuwa na gari" yule mgonjwa akamuangalia docta kisha akamuuliza
Mgonjwa; "docta wewe unavuta sigara"
Docta; " hapana"
Mgonjwa; " sasa gari lako liko wapi?" docta akabaki ameshangaa. "kama sigara huvuti, ungekuwa una gari basi"

0 comments:

Chapisha Maoni