Jumapili, Aprili 27, 2014

JUMA NATURE NA JOKATE MWEGELO KATIKA BEEF YA NDALA

Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Juma Kasim ‘Juma Nature’ wanadaiwa kuacha mshangao kwa wasanii wenzao baada ya kutifuana.

Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga kutomaindi lakini habari za kushangaza zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya ndala au kandambili.
Kabla ya madai haya mapya, Nature aliwahi kunukuliwa redioni wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni.
Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘amekopi’ na ‘kupesti’ wazo lake la biashara.
Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa bila mafanikio.
Nature amekuwa akimpigia simu Jokate lakini haipokelewi
 kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu wa bastola.
Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika kuziona kandambili za Jokate lakini amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa mrembo huyo kamuibia.
Alifunguka: “Hadi sasa hivi sijabahatika kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo langu.

Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu mbaya.
Kweli sikutegemea kama ishu kama hiyo ingefanywa na mtu kama yeye (Jokate) ila hata kama ametoa mimi wazo langu liko palepale.
Nitakuja kuzitoa tu hizo kandambili zenye picha na jina langu.
Baada ya kusikia upande mmoja wa Juma Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na kumsomea mashitaka yake hayo ya kuiba wazo la biashara la Juma Nature.
Bila kupepesa macho wala kuchezesha masikio, Jokate alifunguka kwamba kwa upande wake anasikitishwa na mtu kama Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu anaowaheshimu.
Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake.
Wewe siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo kutoka kwa Nature, niliamini baada ya mimi kutoa hizo ndala, atanisapoti kwani mimi niko katika kuendeleza na kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu letu la maisha.
Kweli Nature amenisikitisha sana kwa kitendo chake cha kunitangazia ubaya.
Hata hivyo, siwezi nikaacha kutoa bidhaa zangu, nitaendelea kutoa ‘so’ itabidi tu anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za kwake
 alisema Jokate, mmiliki wa lebo ya mavazi ya Kidoti.
Wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa ambao walionesha kushangazwa na sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na Nature kuhitilafiana wakati kazi zao zinategemeana.
Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni watu ambao muda wowote wanaweza kukutana kwa ajili ya kufanya kazi,
alisema mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Bongo Fleva.
Kwa mujibu wa mastaa hao, awali Nature aliposikia Jokate ana ‘aidia’ kama hiyo alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii mwenzake hivyo kipato atakachopata kitamsaidia maishani lakini kumbe inawezekana kimoyomoyo ilimuuma ndiyo maana ameendelea kumtuhumu Jokate.
Ni vyema Jokate na Nature wakakaa na kukubaliana waifanye biashara hiyo kwa pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa zaidi, ni kiasi cha kuona fursa na kuitumia.

0 comments:

Chapisha Maoni