HAYA yanaweza kuwa ni mambo ya malovee! Kuna madai kwamba Mbongo Fleva
Nasibu Abdul ‘Diamond’ alishindwa kushiriki zoezi la kuuaga mwili wa
mwanamuziki mkongwe Tanzania, marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed Gurumo
‘Maalim Gurumo’ kwa sababu alifungiwa asitoke ndani na mwandani wake
madam Wema Sepetu, Ijumaa linakudadavulia.
Imedaiwa kuwa, Wema alimfanyia ‘umafia’ mpenzi wake huyo, Aprili 15,
mwaka huu ambapo ilikuwa ndiyo siku ya mwili wa marehemu huyo kuagwa
nyumbani kwake Mabibo jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini Masaki,
Kisarawe, Pwani.
Itakumbukwa kuwa, Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya gari
marehemu Gurumo kutokana na kuguswa na mchango wake katika tasnia ya
muziki nchini.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kitendo cha Diamond kutoonekana katika
mazishi hayo ni kama amejishushia heshima kubwa aliyojijengea pale
alipomthamini marehemu huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota FunCargo.
“Tulitegemea tungemuona msibani lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama
mchango wake wa kumpa gari Gurumo hauna maana,” alisema shuhuda mmoja
aliyekuwepo msibani hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Baada ya mapaparazi wetu kufanya upekuzi yakinifu msibani hapo,
walibaini kuwa, Diamond hakutia ‘maguu’ hivyo shughuli ya kumsaka
ikaanza.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Mapaparazi hawakuchoka, wakahamishia ‘majeshi’ nyumbani kwa
mwanandani wake Wema, Makumbusho, Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa,
Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.
Mapaparazi waliondoka na kurudi tena saa 8:37 mchana ambapo pia
waliambiwa wapendanao hao bado wamejifungia ndani, wakaondoka hadi muda
wa jioni baada ya shughuli za mazishi, walirejea na kuambiwa Diamond
alitoka muda si mrefu pasipo kujulikana alikoelekea.
Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu. Nilikuwa mimi na Diamond tena
tumefika muda huohuo ndiyo mwili ukawa unapelekwa kwenye gari. Huwezi
amini tulijumuika kuupandisha mwili kwenye gari na sisi tukarudi
nyumbani kuendelea na shughuli zetu,” alisema Babu Tale.
Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na maelezo hayo, juzi Jumatano
walimtwangia simu Diamond ambaye alizungumza kwa ‘kujikanyagakanyaga’.
“Mh! Nilikuwepo msibani ila sikwenda kuzika tu maana nilikuwa na Babu
Tale pale na tulikuwa karibu kabisa na gari la Global Publishers, mara
tu baada ya kumaliza kuupandisha mwili wa marehemu kwenye gari
tuliondoka na kurejea kwenye majukumu yetu,” alisema Diamond.
Mapaparazi wa Global walikuwa jirani na gari alilotaja Diamond lakini
hawakumuona staa huyo achilia mbali waombolezaji wengine ambao
waliuliza kwa nini msanii huyo hakufika kwenye msiba wa rafiki yake
mkubwa!
0 comments:
Chapisha Maoni