Rais Jakaya Kikwete, amesema kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa
adabu, kwa baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli
Waanzilishi wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh
Abeid Amaan Karume.
Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao
wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi makubwa na ya kihistoria, kiasi
cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha na kuenzi heshima yao
kwa namna ya kudumu.
Rais Kikwete ametoa msimamo huo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu matusi,
kejeli, dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa
Bunge Maalum la Katiba juu ya waasisi hao wa Tanzania na Wabunifu Wakuu
wa Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni