Jumatatu, Machi 17, 2014

WATU 200 WAMEUAWA NIGERIA

Watu wasiopungua 200 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya watu wasiojulikana  kushambulia vijiji vitatu katikati mwa Nigeria.
Taarifa zinasema kuwa, karibu watu 200 wameuawa baada ya watu wanaobeba silaha kushambulia na kuchoma moto vijiji vitatu vya Ugwar Sankwai, Ugwar Gata na Chenshyi vilivyoko katika jimbo la Kaduna. Taarifa zinasema kuwa, watu waliotekeleza shambulio hilo ni kutoka kabila la Fulani. Afisa mwandamizi wa polisi katika jimbo la Kaduna amethibitisha k
utokea kwa shambulio hilo. Shambulio hilo limetokea katika eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likigubikwa na mapigano ya kidini na ugomvi wa ardhi. Shambulio hilo la jana limetokea katika hali ambayo, siku ya Jumamosi kwa akali watu 212 waliuawa katika mapigano yaliyotokea kati ya jeshi la Nigeria na wanamgambo wa kundi la Boko Haram katika eneo la Maiduguri lililoko katika jimbo la Borno. Taarifa zinasema kuwa, wanamgambo  207 wa Boko Haram na wanajeshi watano wa serikali ya Nigeria waliuawa kwenye mapigano hayo.

0 comments:

Chapisha Maoni