BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu Bongo, Yusuf Mlela
amefunguka kuwa ukimya huo umesababishwa na malezi ya mwanaye.
Akichonga na Fichu Tz, Mlela alisema anahitaji muda mwingi kukaa na
mwanaye Mwantumu kama baba hivyo majukumu yamekuwa mengi, anawaomba
mashabiki wake kuelewa kwani ‘soon’ atakuja kivingine.
“Muda mwingi nautumia kukaa na mwanangu hata yale mambo ya kuzunguka
hovyo kwenye starehe hakuna tena ila pamoja na malezi bado najiiba
kuandaa kazi zangu za filamu na muda siyo mrefu nitaanza kuzitoa,”
alisema Mlela.




0 comments:
Chapisha Maoni