Jumapili, Machi 02, 2014

SUDAN YA KUSINI HAKUKALIKI

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia misaada ya kibinadamu ameelezea  hali mbaya inayowakabili wananchi wa Sudan Kusini.
Valerie Amos ambaye mwezi uliopita alifanya safari nchini Sudan Kusini ameeleza kuwa, licha ya kufikiwa makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi nchini humo, maisha ya mamilioni ya wananchi wa nchi hiyo yamo hatarini kutokana na kuendelea mapigano ya hapa na pale, ukosefu wa chakula na kuibuka maradhi ya milipuko nchini humo. 
Valerie Amos ameongeza kuwa, zaidi ya watu 100 wameuawa wakiwa mahospitalini au makanisani ambako walikwenda kutafuta hifadhi. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kambi za wakimbizi za Umoja wa Mataifa zinawahifadhi wakimbizi wasiopungua elfu ishirini, na kusisitiza kuwa zaidi ya watu laki tisa wameyakimbia makazi yao na wengine laki moja na elfu tisini wamelazimika kukimbilia nchi jirani.

0 comments:

Chapisha Maoni