KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal amedai kuwa
mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United anapata wakati mgumu
kuzoea aina ya soka inayofundishwa na kocha David Moyes.
Kuna taarifa
kuwa Van Persie alikwaruzana na Moyes kutokana na aina ya mazoezi
anayotoa msimu huu huku Shirikisho la Soka la Uholanzi likiwasiliana na
United kuhusu majeruhi yanayomuandama nyota huyo kuelekea katika michuano
ya Kombe la Dunia.
Van Gaal anaamni kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa
Arsenal atakuwa fiti kwa Kombe la Dunia kwasababu mechi za timu ya
taifa ni rahisi ukilinganisha na za United.
Kocha huyo aliendelea kudai
kuwa ana uhakika nyota huyo atang’aa akija katika timu ya taifa kama
alivyofanya katika mechi zao za kufuzu kwasababu ni mahala ambapo
anaweza kucheza kama alivyozoea kulinganisha na klabu yake.
SOURCE: FULLSOKA



0 comments:
Chapisha Maoni