Jumamosi, Februari 22, 2014

CHUCHU HANS NA RAY WAIBULIWA MAPYA, NDOA YAO BADO SIKIO LA KUFA

Ni pigo kubwa! Ile ndoa inayodaiwa kukaribia kufungwa kati ya nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Miss Tanga 2006 aliye pia msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans imepingwa isifungwe mpaka mambo f’lani yakae  sawa.
Kwa mujibu wa mtonyaji wetu, Ray na Chuchu wako mbioni kufunga ndoa wakati wowote kuanzi Mei, mwaka huu, lakini mjadala mzito uliopo mbele yao kwa sasa ni uhalali wake.
“Unajua wanachofahamu wao (Ray na Chuchu) wanaweza kufunga ndoa kwa ulaini kabisa, lakini ukweli ni kwamba kuna ugumu mkubwa.“Kanisa analosali Ray, viongozi wanasema wao si wa dunia hii mpaka wakubali kufunga ndoa ambayo mmoja wa wahusika ana ndoa yake,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “Kwa hiyo kama wako tayari kufunga ndoa hiyo lazima Chuchu akubali kubadili dini yeye ndipo ataruhusiwa kungia kanisani kufungishwa ndoa.”

CHANZO: GPL

0 comments:

Chapisha Maoni