Jumatano, Februari 19, 2014

MAMA WEMA SEPETU AFUNGA AKIOMBA WEMA AMFUMANIE DIAMOND ILI WAACHANE

MAMA wa Miss Tanzania 2006 aliye pia staa wa muvi za Bongo, Wema Sepetu, Mariam Sepetu amesema anamwomba Mungu bintiye huyo amfumanie mpenzi wake asiyemkubali, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza na mapaparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, mama Wema alisema:
“Najua kwa sasa sina tena mamlaka ya kuingilia mapenzi ya binti yangu kwani mambo hayo yamenichosha, yananiumiza na kichwa.
“Lakini naomba sana kwa Mungu itokee siku moja Wema amfumanie Diamond akiwa na mwanamke mwingine labda ndiyo itakuwa kikomo chao cha kuwa wapenzi kwani ndiyo ndoto ninayoiota kila siku.”
Mama Wema alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba, amegundua binti yake huyo hana ubavu wa kuachana na Diamond hata kama atasikia ana mwanamke mwingine.

0 comments:

Chapisha Maoni