Uongozi wa Azam FC kwa niaba ya benchi la ufundi na wachezaji, tunaomba
radhi kwa mashabiki wetu mnaotupenda na kutuunga mkono kwa matokeo
mabovu na mpira mbovu tuliouonesha jana. Mpira na matokeo yale
havilingani na uwekezaji, huduma na matarajio ya wamiliki, wapenzi na
mashabiki wa kweli wa Azam FC, Lengo la uongozi mwaka huu ilikuwa ni
kucheza angalau raundi ya makundi ya mashindano ya kombe la shirikisho
na pia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania. Kwa matokeo ya Beira Mozambique
na jana Chamazi, ni dhahiri ndoto za mashindano ya kimataifa zimekufa
kabisa huku ile ya kutwaa ubingwa wa Tannzania ikiwa rehani.
Azam FC inawaomba radhi watu wote mlioumizwa na matokeo haya na kama
taasisi tutakaa chini, tutajiuliza, tutajitazama, tutajipanga na kuweka
mikakati ya usajili makini ili kuanzia msimu ujao tusiwe na hali ya
kizungumkuti kama hii.
Tunaomba mashabiki wetu muendelee
kutuunga mkono hasa wakati huu tunapoelekea kwenye mechi ngumu ya ligi
kuu dhidi ya Ashanti United jumatano hii
Jumatatu Njema
Imetolewa na Utawala
Jumatatu Njema
Imetolewa na Utawala
0 comments:
Chapisha Maoni