Jumatano, Februari 19, 2014

AJALI MBAYA IMETOKEA MLIMA SEKENKE, LORI NA MTU WATEKETEA KWA MOTO NA KUBAKI MAJIVU...PICHA PIA ZIPO HAPA

LORI la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
 Akiendelea kuongea shuhda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.

0 comments:

Chapisha Maoni