Upinzani huko Ukrain umeapa kutotoka uwanja wa uhuru wanakoendeleza maandamano hayo.
Wakuu kutoka umoja wa Ulaya wameshtumu vikali
rais wa Ukrain Viktor Yanukovych, kwa makabiliano makali baina ya polisi
na waandamanaji yanayoingia siku ya pili sasa .
Waziiri Mkuu wa Poland , Donald Tusk, amesema
atapendekeza Ukrain iwekewe vikwazo vya kiuchumi huku yule wa Sweden
Carl Bildt akiongeza kuwa damu ya watu 25 waliokufa katika maandamano
hayo iko mikononi mwa Yanukovych.
Vile vile wameutaka upinzani kuzuia machafuko zaidi ambayo yanasambaa kwengineko nchini humo.




0 comments:
Chapisha Maoni