IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego wa kujiuza na
makachero wa OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo, Baby Madaha
ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa
amechoshwa na maisha ya presha.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha
alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata
kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho
kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa
upande wake.
SOURCE: GPL




0 comments:
Chapisha Maoni