Tuhuma hizo zinahusishwa na kile kinachosemekana kuwa kashfa ya 'Cashgate' ambapo hadi sasa washukiwa sabini wamekamatwa.
Katika kashfa hii,mamilioni ya dola pesa za serikal ziliibwa kiasi cha kuathiri mishahara ya wafanyakazi wa umma.
Kukamatwa kwa waziri huyo wa zamani, Ralph
Kasambara, ni hatua kubwa katika juhudi za kufumbua kashfa hii ambayo
inasemekana kuwa ngumu kwa serikali.
Alifutwa kazi kama waziri mwezi Septemba na
tangu Novemba mwaka jana amekuwa nje kwa dhamana kwa madai ya kupanga
mauaji ya afisaa mmoja wa wizara ya fedha.
Bwana Kasambara pia alitarajiwa kufikishwa
mahakamanai Jumanne kumtetea mwanamke aliyehusishwa na kashfa hiyo,
hatua ambayo anasema serikali inajaribu kumnyamazisha.
Mashitaka anayokabiliwa nayo ni pamoja na kampuni yake ya sheria kupokea pesa za wizi kutoka kwa serikali
Anakanusha tuhuma hizo akisema kuwa alikuwa waziri wakati huo wala hakuwa mkuu wa kampuni yake.
0 comments:
Chapisha Maoni