WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ZA BARABARANI MKOANI MBEYA.
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA
MATUKIO MAWILI YA AJALI ZA BARABARANI. KATIKA TUKIO LA KWANZA MNAMO TAREHE 26.01.2014
MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA SANTILYA WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI KATIKA BARABARA YA VUMBI MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ELISHA
NONGWA (40) MKAZI WA KIJIJI CHA CHISONDA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.143 ALF AINA YA M/FUSO WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA
KATIKA ENEO HILO. UCHUNGUZI UNAONYESHA KUWA CHANZO CHA AJALI HIYO NI BAADA YA
GARI HILO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA KISHA KUPINDUKA. DEREVA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO,
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KATIKA TUKIO LA PILI, MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA
YA SAA 21:00HRS HUKO ENEO LA BAGAMOYO WILAYANI RUNGWE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LUGANO SIMON (29) MWENDESHA PIKIPIKI YENYE
NAMBA ZA USAJILI T.233 CJA AINA YA BOXER ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU BAADAYA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI
T.309 BM AINA YA TOYOTA DYANA MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI, DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA MATUKIO HAYA
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WATU SITA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUCHEZA KAMARI.
WATU SITA WANASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI MKOANI MBEYA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA WANACHEZA KAMARI HUKO KATIKA
ENEO LA NSALALA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
26.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS EMANUEL SAMWEL (23) AKIWA NA WENZAKE WATANO
WALIKAMATWA WAKICHEZA KAMARI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI. TARATIBU ZINAFANYW A ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA
KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO ISIYORUHUSIWA KISHERIA NA BADALA YAKE WATAFUTE SHUGHULI
ZA KUFANYA ILI WAJIPATIE KIPATA HALALI.
MTU MMOJA ASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI PAMOJA NA SILAHA
MBILI AINA YA GOBOLE.
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA
KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORO WA PORI LA RUNGWE LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
AITWAYE DAUDI CHEREHANI (27) MKAZI
WA BITIMANYANGA BAADA YA KUMKAMATA AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA NYATI UZITO WA KILO TANO [05] PAMOJA NA SILAHA MBILI [02] AINA YA GOBOLE BILA
KIBALI AKIWA NYUMBANI KWAKE. MTUHUMIWA
NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA MARA MOJA UWINDAJI HARAMU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO
KWA JAMII KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA KISHERIA ZA KUMILIKI SILAHA, VINGINEVYO
KWA YEYOTE ANAYEMILIKI SILAHA BILA KIBALI AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni