Jumapili, Januari 05, 2014

UWANJA MAALUM UNAOJENGWA SAO PAULO KWAAJILI YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2014 UMEBOMOKA NA KUUA WAWILI


Watu wawili wamepoteza maisha baada ya kubomoka kwa sehemu ya uwanja mpya wa mpira wa miguu unaojengwa kwenye mji wa Sao Paulo, uwanja mbao ndio unatarajiwa kutumika katika sherehe za kufungua mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Uwanja baada ya kuanguka na jinsi ulivyoharibika
Jinsi uwanja huo ulivyotarajiwa kuwa baada ya kumalizika
Katika tukio hilo watu Wawili walimepoteza maisha, walikua miongoni mwa Wafanyakazi wanaojenga uwanja huo ambapo kubomoka kwa uwanja huu kulitokana na kufeli kwa crane ya chuma iliyokuwa ikitumika kuezekea paa la uwanja huo,ambapo waliofariki ni Fabio Luiz Pereira, 42, driver/operator wa crane ya kampuni ya BHM Munck pamoja na mjenzi Ronaldo Oliveira dos Santos, 44. 
Brazil inajaribu kuhakikisha Viwanja vyote 12 vitakavyotumika kwenye mechi za kombe la dunia vinakamilika na ndio maana vimekua vikijengwa kwa kasi ilikuhakikisha vinamalizika kwa muda uliopangwa na FIFA ambao ni December 2013.

0 comments:

Chapisha Maoni