Chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema kimewafukuza uwanachama aliyekuwa mjumbe Kamati kuu taifa wa chama hicho Dr. Kitila Mkumbo na aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha Samsom Mwigamba.Akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wanachama wa chama hicho jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Chadema Dkt Wilbrod Slaa amesema maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia kikao cha kamati kuu kukaa na wahusika hao na kuwapa nafasi ya kujitetea bila mafanikio ya kuonesha ukweli wa waraka waliouanda na hatimaye kamati ikaamua kuwafutia uwanachama wao.
Aidha Dkt Slaa ameongeza kuwa Dr. Kitila pekee ndiye aliyejitokeza siku ya kujitetea mbele ya kamati kuu na chama chao kilipokea taarifa ya kutojadili uwanachama wa aliyekuwa naibu katibu mkuu wake Mh. Zitto Kabwe kutoka mahakama kuu ya Tanzania na kuwa alichokifanya Mh. Zitto ni kukiuka taratibu na kanuni za chama.
Nao baadhi ya wanachama wa chama hicho licha ya kupongeza hatua iliyofikiwa wamesema hata hivyo maamuzi hayo yamechelewa kutolewa na viongozi wanaokuwa na mipango ya kuharibu taratibu za chama hawafai na kutoa wito kwa hatua kama hizo kuendelea kuchukuliwa dhidi ya viongozi watakaoonekana kufanya hivyo.



0 comments:
Chapisha Maoni