Tukio
hilo lililowagusa wengi, lilitokea juzikati katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee, jijini Dar ambapo mchungaji huyo ambaye hakupenda
kujitambulisha jina lake, alifuatilia shoo ya Shilole kisha akamwita
kumpa darasa la wokovu.
Akizungumzia tukio hilo,
Shilole aliweka plain kuwa, mchungaji huyo aliguswa na namna ambavyo
watu wengi walikuwa wakifuatilia shoo yake, akaona anaweza kuwabadilisha
wengi waliopotea kupitia wokovu.
“Aisee ilikuwa noma, nilipoona
ananiita nilishtuka kidogo. Mbaya zaidi aliniambia anataka tupige picha
pamoja, ndipo alipoanza kunipa darasa la wokovu.
“Alinitaka nibadilike kimavazi, pia nisimsahau Mungu katika maisha
yangu yote na alimalizia kwa kunitaka niende kanisani kwake ili
ikwezekana nitumie uimbaji wangu kuwabadilisha wengi waweze kumtumaini
Bwana,” alisema Shilole staa wa wimbo Nakomaa na Jiji.
Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, Shilole alionekana kuguswa na
maneno ya mchungaji huyo na kusema yamemkumbusha suala la kumkumbuka
Mungu kila wakati katika kazi za mikono yake.
Akasema kwa kuzingatia hilo, sehemu ya mapato yake atakuwa akiyatumia
katika kutoa sadaka husan kwa watu wasiojiweza ili kutimiza amri ya
Mungu.
“Ni wakati wa kubadilika, huu muziki tunafanya upo na utaendelea
kuwepo lakini jambo la muhimu sana ni kumuabudu Mungu katika siku zote
za maisha yetu ya hapa duniani,” alisema Shilole.
0 comments:
Chapisha Maoni