Kumbe kile ‘kibendi’ cha staa wa sinema za Kibongo, Jennifer Kyaka
‘Odama’ ni cha kigogo mmoja serikalini na ndiyo sababu kubwa ya
mwigizaji huyo kufanya siri nzito juu ya ujauzito huo.
Kama mbu aenezavyo ugonjwa wa malaria, ndivyo rafiki wa karibu na msanii huyo alivyotunyetishia juu ya usiri huo huku akisisitiza hifadhi ya jina.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii,
rafiki huyo alisema kwa sauti tulivu kuwa mimba ya Odama ni ya bosi
mkubwa wa moja ya wizara nyeti hapa nchini (jina na wizara vinavunda
kwenye droo zetu) na kwamba moja kati ya masharti magumu aliyompa ni
kuhakikisha jambo hilo linabaki kuwa siri hadi Yesu atakaporudi.
Ilisemekana kuwa usiri huo unatokana na madai kwamba kigogo huyo ni mume wa mtu.
Akiendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi, ‘kikulacho’ huyo alisema licha ya Odama kupata huduma zote bora anazostahili mjamzito lakini hana raha kwani furaha ya mjamzito ni pamoja na kumnadi mhusika wa ‘mzigo’ jambo ambalo limekuwa likimnyima raha.Baada ya kunyetishiwa habari hizo, gazeti hili lilimsaka Odama kupata ukweli juu ya jambo hilo ambapo alitiririka: “Nani kawaambia tena? Aaah, mmnh! Nitawaambia baadaye bwana kwa sasa niacheni kwanza nina mambo yananisumbua, muda ukifika mtajua tu.”Kama kawaida yetu kujiridhisha kwa kina juu ya habari yoyote, kwa pointi hiyo mwandishi wetu alisaka namba za simu ya mkononi ya kigogo huyo na alipopigiwa alijibu kwa kifupi: “Niko kwenye kikao tuma meseji.”
Licha ya mwandishi wetu kutuma ujumbe mfupi wa madai hayo kwa simu lakini kigogo huyo hakujibu chochote hadi gazeti hili ‘linajipeperusha’ kwenda mitamboni kuchapishwa, hivyo jitihada za kunasa undani zaidi wa habari hii zinaendelea.

0 comments:
Chapisha Maoni