Naibu Waziri Mkuu wa Libya amenusurika jaribio la kutaka kumuua katika mji mkuu Tripoli.
Al Sidik Abdul Karim alishambuliwa na watu wasiojulikana hapo jana
akiw
a ndani ya gari, shambulio linalodhihirisha vurugu na machafuko
yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo. Mwanzoni mwa mwezi huu pia Naibu
Waziri wa Viwanda wa Libya Hassan al Droui alishambuliwa na kuuawa
katika mji wa Sirte.
Tangu dikteta Muammar Gaddafi ang’olewe madarakani mwaka 2011,
serikali ya Libya imeshindwa kudhibiti makundi ya wanamgambo ambao
walishiriki kumpindua Gaddafi, huku silaha zikizagaa ovyo mikononi mwa
raia.
0 comments:
Chapisha Maoni