Mjumbe maalum wa Marekani katika Maziwa makuu,amesema kuwa
hali ya usalama katika eneo hilo inaendelea kuimarika, baada ya waasi wa
kundi la M23 kukubali kusalimisha silaha mwezi Novemba.
Akiongea baada ya ziara yake ya siku tisa nchini humo, Russell
Feingold alisema kuwa baada ya M23 kukubali kusitisha vurugu hizo za
zaidi ya mwaka mmoja, makundi mengine ya waasi pia yalihitaji
kusalimisha silaha zao.
Lakini ameongeza kuwa wakati changamoto nyingi bado zipo, nchi hiyo
imepiga hatua ya kwanza katika kuimarisha hali ya usalama nchini humo.
Wakati huohuo, mapigano makali yameibuka Jumanne,kati ya jeshi la serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo na waasi wa ADF.
Kufuatia mapigano hayo vijiji vya Amisi na Nadwui vilivyokuwa ngome za waasi wa ADF vimechukuliwa na vikosi vya serikali.
Vijiji hivyo viko kilometa takriban 100, kutoka mji wa Beni.
Wakazi wa maeneo hayo wamefurahia kurejeshwa kwa vijiji hivyo mikononi mwa jeshi la serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni