Jumatatu, Januari 27, 2014

MAURINHO: IMENIWIA VIGUMU SANA KUMWACHIA MATA!

Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesmea kuwa ulikuwa ni ‘uamuzi mgumu’ kwake kumwachilia mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Uhispania Juan Mata kujiunga na wapinzani wao katika ligi kuu ya England Manchester United.
Mata aliye na umri wa miaka, 25, ameandikisha rekodi ya uhamisho katika klabu ya Man United kwa baada ya kuuzwa na Chelsea kwa kititia kinono cha pauni milioni 37.1.
Mourinho amesema: ” Haya ni maamuzi ambaye mkufunzi anapaswa kufanya, lakini kwangu ilikuwa vigumu. Ningependa kuendelea kumwona katika kikosi changu bila shaka,”
“Lakini kuwa katika hali hii kwa mchezaji ni vigumu. Anastahili kuachiwa milango wazi katika Chelsea. Napenda kuwaona watu wakiwa na raha. Nasikitika sikuweza kumfurahisha katika kikosi hiki – nasikitika sana kwa hilo, lakini najenga kikosi changu nikizingatia mchezaji Oscar ambaye anacheza katika nafasi ya 10,” anasema mzee Mourinho.

0 comments:

Chapisha Maoni