Jumatatu, Januari 27, 2014

DROO YA MICHUANO YA KOMBE LA FA

Droo ya michuano ya kombe la FA imefanywa kwa mechi za mchujo wa raundi ya tano.
Chelsea wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo unaotazamiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Droo kamili:
  • Manchester City v Chelsea
  • Sheffield United au Fulham v Nottingham Forest au Preston North End
  • Arsenal v Liverpool
  • Brighton & Hove Albion v Hull City
  • Cardiff City v Wigan Athletic
  • Sheffield Wednesday v Charlton Athletic
  • Sunderland v Southampton
  • Everton v Swansea City
Chelsea ambao wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii amesema, “Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.”
Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.

Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.
Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.
Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.
Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainal yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.

0 comments:

Chapisha Maoni