Klabu ya Manchester City imechupa hadi kileleni mwa
ligi kuu ya soka nchini England baana ya kuonesha soka safi dhidi ya
klabu ya Tottenham katika uga wa White Hart Lane.
Kikosi cha kocha Manuel Pellegrini kilihitaji
ushindi dhidi ya Spurs ili kuwapiku Arsenal kwenye jedwali la msimamo wa
ligi hiyo, na matumaini hayo yalianza kuonekana mapema wakati Aguero
alipovuna bao la kwanza, hii ikiwa ni mara ya nane mfululizo akiifungia
City katika mechi nane mfululizo.
Yaya
Toure aliiweka Man City kifua mbele kwa bao la pili, dakika ya tano
kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penalti uliozua utata ambapo mlinda
ngome wa Spurs Danny Rose alitimuliwa uwanja kwa kulishwa kadi nyekundu
japo alionekana kuugusa mpira kwanza kabla ya kuadhibiwa kwa kumchezea
rafu Edin Dzeko.
Dzeko aliongeza bao la tatu na ingawa Etienne
Capoue alifunga bao la kufuta machozi kwa Spurs, bado kulikuwa na fursa
kubwa kwa Man City kuendelea kuinyeshea Spurs mvua ya magoli kupitia
mchezaji wa akiba Stevan Jovetic aliyefunga bao lake la kwanza katika
ligi kuu tangu uhamisho wake wa pauni £22m kutoka klabu ya Fiorentina ya
Italia.
Aguero afunga mabao 50
Baada ya mechi hiyo Sergio Aguero sasa
ameandikisha rekodi ya kufunga takriban mabao 50 ya ligi kuu baada ya
mechi 81, na kuibuka kuwa mtu wa tano kufunga kiasi hicho cha mabao,
baada ya Andy Cole, Alan Shearer, Ruud van Nistelrooy na Fernando
Torres.
Kisha City ikaongeza maumivu zaidi kwa Spurs
baada ya kile kipigo cha mabao 6-0 mwezi November mwaka uliopita, pale
Vincent Kompany alipokamilisha kibarua kwa kufunga bao la tano na la
ushindi.
Chelsea 0 - 0 West Ham
Kwenye matokeo ya mechi nyinginezo Chelsea
ilipata pigo kwenye harakati zake za kutafuta uongozi kwenye jedwali
baada ya kulazimika kutoka sare ya kutofungana na West Ham katika uwanja
wa nyumbani Stamford Bridge.
Kwingineko Aston Villa iliishinda West Brom mabao 4 - 3 nayo Sunderland ikainyuka Stoke 1-0.
Kwingineko Aston Villa iliishinda West Brom mabao 4 - 3 nayo Sunderland ikainyuka Stoke 1-0.
Hii ndiyo orodha ya saba bora tarehe 30-01-2014:
1 Man City 53
2 Arsenal 52
3 Chelsea 50
4 Liverpool 46
5 Tottenham 43
6 Everton 42
7 Man Utd 40
2 Arsenal 52
3 Chelsea 50
4 Liverpool 46
5 Tottenham 43
6 Everton 42
7 Man Utd 40
0 comments:
Chapisha Maoni