Jumatano, Januari 29, 2014

HALI YA MICHAEL SCHUMACHER NI MAHUTUTI

Mwezi mmoja baada ya kujeruhiwa katika ajali ya mchezo wa kuteleza kwenye barafu, meneja wa jogoo wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga, mjerumani Michael Schumacher ameiambia BBC kwamba madaktari wanaendelea kumweka katika hali ya 'kuzirai kimatibabu', na kwamba yuko katika hali imara.
Bingwa huyo mara saba aligonga kichwa chake dhidi ya mwamba wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Madaktari wanatumia madawa kumpa usingizi wakijaribu kupunguza uvimbe na kuchubuka kwenye ubongo wake.
Tayari wametekeleza upasuaji mara mbili kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo.
Hata hivyo huenda maisha yake yakawa hatarini iwamo ataendelea kuwa katika hali ya kuzirai kutokana na hatari ya ubongo wake kuharibika na kupata maambukizi ya kifua.

0 comments:

Chapisha Maoni