Mafuriko hayo
yalisababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha Jumatano iliyopita na
kusababisha maafa makubwa yakiwamo kuharibiwa kwa makazi ya watu,
majengo ya serikali zikiwamo shule, vyuo na mahakama.Shuhuda wa tukio
hilo, Lugendo Seleman, mkazi wa Kijiji cha Magole Tarafa ya Dumila
Wilaya ya Kilosa mkoani hapa alimuonyesha mwandishi wetu gesti ambayo
jamaa aliyefahamika kwa jina moja la Kashinde, mkazi wa kijiji hicho
ambaye alikurupuka kuokoa maisha yake akiwa na mke wa mtu.
“Za mwizi
kweli 40, Kashinde katoka gesti uchi wa mnyama na kupiga mbizi akiwa na
mke wa mtu ambaye mumewe amesafiri muda mrefu yuko mjini akisaka maisha
na ana kama miezi 6, huwa anakuja na kuondoa hivyo mkewe amekuwa na
uhuru,” alisema Seleman na kuongeza:
“Umechelewa kidogo tu ungepata picha zao yeye na mke huyo wa mtu
wakipiga mbizi uchi wa mnyama wakitokea gesti, sijui jana usiku walilewa
sana mpaka wamechelewa kuamka na kukutwa na mafuriko, muda huu wa saa
nne asubuhi!”
Aidha, juzi Alhamisi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi,
John Magufuli walifika eneo hilo la tukio na kujionea hali halisi.
Akizungumza na wananachi wa Kijiji cha Magole, Pinda aliwaambia
serikali imetoa chakula kwa waathirika wa tukio hilo na kuwataka wanachi
kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kigumu walichopitia.
0 comments:
Chapisha Maoni