Ijumaa, Januari 24, 2014

MABAYA YA DIAMOND PLATINUMZ

AJE aje mapipo, kama kawa kama dawa. Kupitia segimenti hii tutakuwa tukipeana michapo ya hapa na pale iwe info za bigi apu au hata michano kiroho safi kabisa. Ama nini? Basi mia!
Tudei siyo kesi kama vipi ngoja nimtemee madini Diamond, anayetamba na songi la Mai Namba Wani. Kabla sijazama fronti ngoja ninate na biti dakika sifuri.
“Mai switiswiti…mai bebiooo, roho yangu kwako…ngololo, aaah ngololo…ai weee,” mwisho wa biti.
Turudi kwenye mchongo wa siku, machizi kitaa wanammaindi kinoma. Wanasema anazingua kwenye michongo ya mashori, ofukozi ni ishu  yake ya kutoonesha msimamo wa kuseto na manzi mmoko.
Mwanangu Wile juzikati aliniendea mahewa na kunitonya kama vipi nimpe maujanja ya kuseto ili maraia wake wampe marespekti yanayoendana na gemu lake analolisongesha. Hebu tujiunge na mwanangu Wile dakika moko:
“Mwana anasomeka kinoma, watoto wa uswazi na wa kishua wanamuelewa. Tatizo ni moko tu, totozi sana! Kwa nini asiseto kwa shori mmoko akafaiti laifu? Au anadhani laifu la kibachela ni la foreva? Hajui kama siku moko atatakiwa kuitwa mshua? Machalii mjengoni wamwite dingi?”

Mwanangu Wile umetisha sana na amesomeka. Kimsingi amebonga maneno yenye meseji kinoma. Nampa gwara mwana, ametema cheche ambazo zinaweza kuwa za shombo bati ndo mpango mzima.
Kuwa na msimamo kwenye laifu ndiyo mpango. Tudei huwezi kuwa na shori huyu, ukasavaivu naye kisha ukammwaga kwa mbwembwe pale kati dheni baadaye unarudisha majeshi. Siyo mpango, anazingua.
Wanangu wenyewe mnajua, mchizi alipiga mbizi sana kipindi f’lani na Byutifuli Onyinye, malovee yalikuwa kwenye mstari ileile bati baadaye akampiga chini. Eeee…bana eeeh, si mnakumbuka pale Mlimani Siti alivyochomoa kupokea mtonyo wa Onyinye baada ya kumwagana naye?
Kama hiyo haitoshi, mchizi alipokuwa kakolea katika malovee ya mtoto Peni nini na nini alidaiwa kuchukua kitu cha foni na kumrekodi Onyinye alipokuwa akiomba chansi ya kimalovee. Shai kinomanoma.
Huku na huku nini kitenesi kikadunda tena, akaamua kumpiga chini tena Peni. Bishosti aliyekuwa ameshakita kambi nyumba moko na maza mzazi. Nishai kweli kwa mwana.Wakati wana wanaendelea kumsikilizia kitaa, mwana akarudisha majeshi kwa Onyinye. Tena nasikia kakolea kinoma kiasi cha kushindwa hata kupokea foni za michongo ya mawe. Anayo ya kutosha?
Ila siyo ishu mwisho wa siku kila mtu atabaki kuwa na laifu lake, mimi hapa naweka nukta kwa kumpa maushauri. Msimamo ndo mpango katika laifu.
Miamia wana, tutamiti hapa neksti

SOURCE: GPL

0 comments:

Chapisha Maoni