Ijumaa, Januari 03, 2014

BASHIR AL-ASSAD NA TUMAINI LA SYRIA YENYE NGUVU

Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, nchi yake itaushinda mgogoro wa sasa unaochochewa na kuungwa mkono na madola ya kigeni na kwamba, nchi hiyo itazidi kuwa na nguvu. 
Rais Assad amesema hayo katika mazungumzo yake mjini Damascus na ujumbe wa wataalamu wa Kiislamu na kusisitiza kuwa, hali ya sasa ya Syria ni bora kuliko huko nyuma na kwamba, nchi hiyo itafanikiwa kukivuka kwa ushindi kipindi hiki cha
mgogoro na kuwa na nguvu zaidi. Rais wa Syria amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo linapambana kiume na magaidi wenye kufurutu ada na kusisitiza kwamba, binafsi anaamini kuwa, nchini Syria kuna vita vya kweli dhidi ya wanamgambo matakfiri wa Kiwahabi. Wakati huo huo, Wail al-Halqi, Waziri Mkuu wa Syria amesema kuwa, mwaka huu wa 2014 utakuwa mwaka wa ushindi wa nchi hiyo dhidi ya magaidi.
Waziri Mkuu wa Syria amezikosoa vikali nchi zinazowaunga mkono wanamgambo wanaopigana dhidi ya serikali ya Damascus. Aidha Waziri Mkuu wa Syria amewapongeza wananchi wa nchi hiyo kutokana na kusimama kwao kidete dhidi ya makundi ya kigaidi na kusisitiza kwamba, mwaka huu utakuwa mwaka wa amani na uthabiti kwa nchi hiyo ya Kiarabu.

0 comments:

Chapisha Maoni