MASHABIKI wa Michael Schumacher leo walimtumia salamu za kuadhimisha
kutimiza mwaka wa 45 tangu kuzaliwa kwake wakati akiwa amelazwa
hospitalini kutokana na kujeruhiwa vibaya kichwani wakati alipokuwa
akishiriki mchezo wa kuteleza kwenye barafu maeneo ya Alps nchini
Ufaransa.
Schumacher ambaye ni mshindi wa mara kadhaa wa mbio za kuendesha
magari za Formula One (F1) hivi sasa anapata matibabu akiwa hajitambui
baada ya kufanyiwa operesheni ya kichwa ambapo alikipigiza kwa bahati
mbaya kwenye jiwe.
Schumacher ambaye mashabiki wake humwita Schumi, ndiye dereva mwenye
mafanikio zaidi katika mashindano ya F1 akiwa ameshinda mara 91 kabla
ya kustaafu mwaka 2012.




0 comments:
Chapisha Maoni