Alhamisi, Oktoba 17, 2013

SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA TAIRI, GENERAL TYRE ARUSHA NA VINGINE VINGI



Serikali imeeweka mikakati ya kufufua viwanda vya kati, ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Tairi (General Tyre Arusha).

Maandalizi ya Awali ya ufufuaji wa kiwanda hicho yameshaanza, ikiwa ni pamoja na mashamba ya mpira ya kihuhwi - Muheza (hekta 789) na kalunga - kilombero (Hekta 750).
Katika mwaka wa fedha 2013/14 serikali imetenga sh. Bilioni 6.3 kwa ajili ya ukarabati wa majengo na mitambo ya kiwanda, na kufufua mashamba ya mpira.
Mradi huu unatarajiwa kutoa AJIRA kwa watu Takriban 500.

0 comments:

Chapisha Maoni