Alhamisi, Oktoba 17, 2013

KAULI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KUHUSU UKAGUZI WA RUZUKU ZA VYAMA VYA SIASA.

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kutoa taarifa zinazoshutumu kuwa vyama vya siasa nchini havijafanyiwa ukaguzi wa mahesabu kwa muda mrefu, CCM imeibuka na kuitwisha Chadema tuhuma hizo.
Imesema yenyewe (CCM) imekuwa ikiitika mwito wa sheria hiyo na kwamba hesabu zake zimekuwa zikikaguliwa kwa miaka mingi sasa, hata kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini. Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema, ni sahihi kwa hesabu za vyama vya siasa kukagukiwa kwani ni kwa mujibu wa sheria, na ndiyo sababu CCM imekua ikitekeleza sheria hiyo kwa miaka mingi hata kabla ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa. Nape alisema, badala yake chama kinachopaswa kutiliwa shaka kuhusu ukiukaji wa sheria hiyo, ni Chadema, chama ambacho alidai kimekuwa na tabia ya kufanya mambo mengi kinyume cha sheria kwa kisingizio cha mwavuli wa siasa.

0 comments:

Chapisha Maoni