Alhamisi, Oktoba 17, 2013

JB AKANA CHIPUKIZI KUSAFIRIA NYOTA YAKE

JB alisema yuko tayari kuendeleza kipaji cha msanii ambaye tayari ameshaanza sanaa akiwa na kipaji cha kweli na hana tamaa ya umaarufu na si wimbi kubwa la wasanii ambao wana uchu wa kusaka umaarufu kupitia sanaa.
“Hata watu wanichukie mimi sijali kwani kipaji cha kweli kinaonekana dhahiri na huwa sipendi kumpa mtu umaarufu wakati hana kipaji, kimsingi nipo kwa ajili ya kuendeleza kipaji, sitaki kuwabebabeba chipukizi ili watoke kupitia jina langu,” alisema JB na kuongeza:
“Unaweza kubebwa leo kwa lengo la kuonekana katika runinga kwa kipindi kifupi lakini baada ya muda unapotea, sasa hapo itakuwa na maana gani si bora nisiwasaidie kabisa kuliko kuwabeba wasiobebeka.”

0 comments:

Chapisha Maoni