Msemaji wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza tena kuwa, amani haitopatikana katika eneo hadi pale nchi huru ya Palestina itakapoundwa, mji mkuu wake ukiwa Baitul Muqaddas Mashariki.
Nabil Abu Rudainah amesema hayo katika kujibu ripoti ya hivi karibuni ya shirika la Israel la 'Amani Sasa' lililotangaza kuwa, njia pekee ya kupatikana amani katika eneo ni kuundwa nchi huru ya Palestina katika mipaka ya mwaka 1967, mji mkuu wake ukiwa Quds.
Abu Rudainah ameongeza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Palestina ni kinyume cha sheria na maazimio ya kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti za shirika hilo la 'Amani Sasa' ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki katika kipindi cha nusu ya mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 70 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

0 comments:
Chapisha Maoni