WILAYA YA MBEYA MJINI -
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO MWANJELWA BARABARA YA
MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. GARI T.387 BMN AINA YA
TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA
DEREVA HANSI S/O HUMPHREY, MIAKA
37, KYUSA, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA
MTEMBEA KWA MIGUU WESTON S/O HEPA
MWALINGO, MIAKA 83, MSAFWA, MKAZI WA
AIRPORT NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MPANDA
PIKIPIKI KUMGONA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO MBALIZI BARABARA YA TUNDUMA /MBEYA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
REUBEN S/O MWAKALOBO, MIAKA
22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI TEULE YA IFISI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA PIKIPIKI AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI TEULE YA IFISI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA PIKIPIKI AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA
YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA
20:00HRS HUKO KATIKA ENEO KYELA KATI WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LUGANO S/O RICHARD, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA,
MKAZI WA KYELA – KATI AKIWA NA BHANGI GRAM 20. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO
WA SURUALI YAKE. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA BAR IITWAYO NURU INN ENEO LA MBALIZI WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. ALIKAMATWA ERICK S/O JAMSON, MIAKA 25, MSAFWA, MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA NOTI BANDIA
MOJA YA TSHS 10,000/= YENYE NAMBA – DT 2937833. MBINU NI KUTAKA KUNUNUA VINYWAJI KWA
KUTUMIA PESA HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII HASA KATIKA MAENEO YA KIBIASHARA KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA PESA ILI KUJIEPUSHA NA WATU WANAOTUMIA PESA
BANDIA . AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTANDAO WA WATU WANAOMILIKI PESA BANDIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed
by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni