Jumapili, Septemba 01, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 31. 08. 2013.



 WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA SAA 22:00HRS HUKO KATIKA KJIJI CHA WELU – TWO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. JAMES S/O SHENANGA MWAZEMBE, MIAKA 63, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA WELU – TWO ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWA CHOTE KUSAMBALATISHWA PAMOJA  NA MKONO WA KULIA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU NI KUMVAMIA AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE HUKU MKE WAKE ENITHA D/O NSWIMA, MIAKA 40, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA WELU – TWO AKIWA AMELALA CHUMBA KINGINE NA ALIKUWA AMEFUNGIWA MLANGO KWA NJE KABLA YA  MAUAJI HAYO KUFANYWA. HAKUNA KITU KILICHOCHUKULIWA. CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI   ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA TABIA YA  KUSADIKI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI WATUHUMIWA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

WILAYA YA MBOZI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                            KUSABABISHA KIFO.


MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO ENEO LA OLD – VWAWA BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.606 CEJ/T.625 CHF AINA YA  HOWO LIKIENDESHWA NA DEREVA JUMA S/O SAMIRI, MIAKA 40, MZIGUA,  MKAZI WA DSM LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ENOCK S/O MWAZEMBE, MIAKA 22, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA OLD-VWAWA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA  WILAYA YA  MBOZI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO KWA  MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI - AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                                    KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO ENEO LA MBALIZI BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T.214 BYM AINA YA  T/COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA BONIFACE S/O WAMALWA, MIAKA 38, KYUSA,  MKAZI WA NZOVWE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ENEA D/O DAUA, MIAKA 70, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA NZOVWE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. CHANZO MWENDO KASI.  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO KWA  MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  MBEYA MJINI – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                                   KUSABABISHA KIFO.

.
MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 20:30HRS HUKO ENEO LA UYOLE STENDI YA TUKUYU BARABARA YA MBEYA /TUKUYU JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ALEX S/O MWAKITALIMA, MIAKA 21, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. CHANZO MWENDO KASI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO KWA  MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.      AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA  AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.


WILAYA YA MOMBA – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  1.MASUMBUKO S/O LAZARO MWALYOBE, MIAKA 21, MUWANJI, DEREVA  MKAZI WA KIJIJI CHA IHANDA 2. OBEDI S/O ZABRON PESAMBILI, MIAKA 20, MMALILA, MKULIMA, MKAZI WA UNYAMWANGA - TUNDUMA NA 3.ISMAIL S/O BARTON MAARIFA, MIAKA 25, MSAFWA, BIASHARA, MKAZI WA MTAA WA MWAKA   WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 250. WATUHUMIWA NI WAVUTAJI NA WAUZAJI WA BHANGI. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO MWEUSI WA RAMBO WAKIWA KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA MALI YA  ISMAIL S/O BARTON MAARIFA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.KAIMU  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI   ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA KYELA KATI   WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  EMANUEL S/O IDANI, MIAKA 27, KYUSA,MKULIMA  MKAZI WA KIJIJI NDANDALO  AKIWA NA BHANGI  KETE 91 NA MISOKOTO 10 SAWA NA UZITO WA GRAM 505. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.KAIMU  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI   ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


WILAYA YA MBOZI – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 12:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA MLOWO   WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA  JOSEPH S/O NZUNDA, MIAKA 26, MNYIHA,MKULIMA  MKAZI WA MLOWO   AKIWA NA BHANGI  KETE 200 SAWA NA UZITO WA KILO MOJA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI   ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

WILAYA YA MBOZI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

MNAMO TAREHE 30.08.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MLOWO   WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA PILI D/O MWASHIUYA, MIAKA 32, MNYIHA, MKULIMA MKAZI WA ILOLO   AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI   ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


Signed by:
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Chapisha Maoni