Wazazi na wananchi wa kata ya majengo mkoani hapa wametakiwa kuonesha upendo kwa watoto na kuwajali ili kuepusha ongezeko la watoto wa mitaani.
Akiongelea suala hilo ofisini kwake kiongozi msaidizi wa kituo cha HOPE FOR THE FUTURE FOUNDATION, AMANI GEORGE .amesema ukosefu wa upendo wa wazazi kwa watoto na kutowajali kunachangia kwa watoto hao kukimbilia mitaani.
Amesema wao huwasaidia watoto wa mitaani KWA kuwapa huduma ya vifaa vya shule,chakula,elimu na michezo kwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo.
Hata hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa jamii,taasisi binafsi za kiserikali katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
0 comments:
Chapisha Maoni