Hali ya uchafu katika maeneo kuzunguka masoko bado ni tatizo kubwa katika baadhi ya maeneo ya manispaa ya jiji la Mbeya.
Aidhaa dampo la soko la Ilemi kata ya Isanga limejaa uchafu barabarani kiasi cha kufanya mwonekano wa mazingira hayo kuwa mbaya.
Wakizungumza na Fichuo Tz baadhi ya wananchi wameeleza kuwa dampo hilo limekuwa likisahaulika mara kwa mara na kusababisha baadhi ya watu kuchukukilia eneo hilo ni la uchafu siku zote.
Hata hivyo,baadhi ya watu wa eneo hilo wameendelea kufanya biashara katika mazingira machafu huku wakiuza mazao ya chakula hali inayo hatarisha afya za watumiaji wa mazao hayo.
Nao wakazi wa eneo hilo wameendelea kuilalamikia manispaa ya jiji kwa kusema imekuwa ikiwasahau katika shughuli za utoaji wa taka katika vituo vya ukusanyaji taka.
0 comments:
Chapisha Maoni