Mama wa Trayvon Martin, kijana Mmarekani mweusi
aliyeuliwa Florida mwaka jana wakati akielekea nyumbani, anasema kufutwa
kwa kesi ya mwanamgambo wa kulinda mitaa aliyemuuwa kumewafanya vijana
wengi weusi wa Marekani kuwa waoga.
Akizungumza na BBC, Sabrina Fulton, alitoa wito
sheria inayoruhusu kutumia nguvu ya kuweza kuuwa iwapo maisha yako yako
hatarini - anataka ibadilishwe katika jimbo la Florida na kwengineko
Marekani.
Bi Fulton amepangwa kuhutubia maandamano
yanayofanywa mjini Washington kuadhimisha miaka 50 tangu maandamano
maarufu yaliyofanywa mjini humo kudai haki za watu weusi na ambayo
yaliongozwa na kuhutubiwa na Martin Luther King.
0 comments:
Chapisha Maoni