Jenerali wa daraja ya juu wa Iran ameionya Marekani
kwamba matokeo yanaweza kuwa mabaya iwapo Marekani itapindukia ule
aliosema "mstari mwekundu" nchini Syria.
Matamshi hayo ya naibu mkuu wa jeshi la Iran,
Massoud Jazayeri, yalichapishwa baada ya Rais Obama na waziri mkuu wa
Uingereza, David Cameron, kukubaliana kwamba inafaa kujibu kwa uzito
iwapo itagundulikana kuwa Syria ilitumia silaha za kemikali dhidi ya
watu wake.
Syria imekanusha kuwa ilihusika na lile
linalodaiwa kuwa shambulio lilofanywa Ghouta karibu na Damascus juma
lilopita, ambapo silaha za kemikali zilitumiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni