Alhamisi, Agosti 29, 2013

POWERTILLER LAUA 1 NA KUJERUHI 1 MBEYA


Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa katika ajali ya powertiller juzi majira saa 12:30 jioni huko katika kijiji cha Ukwavila wilaya Mbalali mkoani Mbeya.

 

Habari toka kwa jeshi la polisi zinasema kuwa powertiller aina ya Kubota hilo lililopata ajali lilikuwa likiendeshwa na Medrick Komisimbili, 22, Msanguna mkazi wa Ukwavila lilidondosha watu wawili na kusababisha kifo Scholar Mwanjunju 36, Msangu, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Ukwavila na majeruhi kwa Salima Mpali 20, Msangu, Mkulima na mkazi wa Ukwavila.

Aidha habari hizo zimesema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa lakini Majeruhi amelazwa katika hospitali ya misheni Chimala na mwili wa marehemu umekwisha fanyiwa uchunguzi na daktari na kukabibidhiwa ndugu kwa mazishi.

0 comments:

Chapisha Maoni