Alhamisi, Agosti 29, 2013

AUAWA KWA KUPIGWA NA JIWE KICHWANI MBEYA

Mtu mmoja amefariki dunia katika hospitali ya wilaya ya Chunya jana saa 6:30 mchana baada ya kupigwa na jiwe kichwani katika kijiji cha Igundu, Chunya mkoani Mbeya.
Marehemu amefahamika kwa jina la Said Petro, 45, Mmang’ati, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Igundu amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya baada ya kupigwa na jiwe kichwani tarehe 26/08/2013 majira ya saa 06:01 usiku katika kijiji cha Igundu na mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Mashaka Mayunga, 23, Mngoni,mkulima na mkazi wa kijiji cha Igundu. 
Habari zinaeleza kuwa chanzo cha ugomvi uliotokea kati ya marehemu ni ulevi wa pombe kilabuni na tayari mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani bado zinaendelea wakati mwili wa marehemu umekwisha fanyiwa uchunguzi na daktari wa serikali na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi. 
Pamoja na hayo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na anatoa wito kwa jamii kuachana na tabia ya kunywa pombe kupita kiasi ili kuepusha maatatizo yawezayo kuepukika.

0 comments:

Chapisha Maoni