Jumuiya na Taasisi za kidini ya
Kiislamu nchini Tanzania imeitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina ili
kubaini na kuwachukulia hatua watu waliompiga risasi Sheikh Ponda Issa
Ponda Jumamosi mjini Morogoro Mashariki mwa nchi.
Sheikh huyo ambaye amekuwa katika mivutano ya
mara kwa mara na serikali ya nchi hiyo alipigwa risasi baada ya kutokea
vurugu kwenye mkutano wa mawaidha ya baraza la sikukuu ya idd el fitr.Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Alhajj Mussa Kundecha, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam Jumapili jioni kuwa endapo serikali haitachukua hatua itakayowaridhisha Waislamu, wataamua kufikiria upya mustakabali wao na serikali ya Tanzania.
Sheikh Ponda amelazwa katika hospitali ya taifa, Muhimbili, mjini Dar es Salaam kwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu.



0 comments:
Chapisha Maoni