Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amemtaka Katibu Mkuu wa TFF, Angetile
Osiah kuacha kuzungumzia suala la Mrisho Ngassa na badala yake aiache Kamati ya
Sheria, Haki na Hadhi ya wachezaji ifanye kazi yake na kutoa uamuzi kwa haki.
Kauli ya Rage imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Osiah kukaririwa na Star
TV akisema viongozi wa Simba na Yanga wamekuwa wakifanya usajili kwa kukomoana.
“Simba na Yanga wamekuwa wakifanya mambo kwa kukomoana, kama hili mchezaji
alishaonyesha wazi hahitaji kuchezea klabu yako kwa nini umng’ang’anie
kumsajili, mchezaji kama hataki kucheza klabu yako achana naye toa nafasi kwa
wachezaji wengine, wao wanafanya hivi halafu baadaye waangushe lawama kwa TFF
wanapendelea klabu fulani, kamati itakaa na klabu anayostaili Ngassa kuchezea
basi ataidhinishwa huko.
Hata hivyo Simba imesema haipo tayari kumng’ang’ania mchezaji huyo iwapo
Yanga itatoa kitita cha Sh150 milioni, lakini si chini ya hapo na kwamba wao
wana mkataba na Ngassa ambao utamalizika Mei mwakani.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hans Pope alisema “Mkataba
wetu na Ngassa upo wazi tena unasema wazi utaanza pale ambapo mkataba wake na
Azam utakapomalizika, hatujaingia mkataba juu ya mkataba kama Yanga
wanavyodhani na tuliupeleka TFF toka Desemba mwaka jana.
Ngassa amejikuta kwenye mgogoro wa usajili ambao hatima yake itaamuliwa
Jumanne ijayo na Kamati ya Alex Mgongolwa .
0 comments:
Chapisha Maoni