Wachezaji zaidi ya watano wa timu ya soka ya Yanga wameshindwa kufanya mazoezi leo na timu hiyo baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya timu ya costil union na badala yake wachezaji wachache kujitokeza katika mazoezi hayo.
Zile dakika 90 za mchezo wa yanga na coastil union zilikuwa ni dakika 90 za mateso ya mioyo ya mashabiki wa timu zote mbili,zilikuwa ni dakika 90 za maumivu makali kwa wasukuma ndinga waliyopo uwanjani,dakika zilizoratibiwa na mwamuzi mzowefu martini saanya zilizoacha alama katika soka tanzania na kuwaacha baadhi ya wachezaji na hata mashabiki matozi yakimwaika.
Yanga inayoonekana kutokuwa na babaiko kwasasa imeendelea na mazoezi hii leo huku wachezaji 7 wakiwa nje ya mazoezi hayo kutokan na majeraha huku tff na kamati zake zikibembelezwa kutoa adhabu mwa mwamuzi huyo Moja kati ya mazingaumbwe`yaliyoonyeshwa na mwamuzi huyo ni pale alipotoa kadi ya njano kwa mchezaji wa timu ya costil union bila kuona kosa alilotenda mchezaji huyo na hata bila kuuliza kwa mwamuzi wa pembeni.
0 comments:
Chapisha Maoni