Habari toka kwa maafisa wa polisi zinasema kuwa gari lenye namba za usajili T.855 ACJ aina ya MITSUBISHI FUSO lililokuwa likiendeshwa na dereva CLEMENT EXAVERY, liliacha njia na kupinduka kasha kusababisha kifo cha LAUDEN MWAMPANGALA,17, MKULIMA, MNYIHA na MKAZI wa NAMBIZO na kuwajeruhi wengine 9 ambao wamelazwa katika hospitali ya MBOZI MISHENI.
Aidha habari toka polisi zimesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika zahanati ya kijiji cha NAMBIZO wakati chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni mwendo kasi. Dereva anashikiliwa na jeshi la polisi wakati taratibu za kumfikisha mahakamani zikiendelea kufuatwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa MBEYA na Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi DIWANI ATHUMANI ametoa wito kwa madereva kuwa makini kipindi watumiapo vyombo vya moto kwa kuzingatia usalama wa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika
0 comments:
Chapisha Maoni