Leo ni Alkhamisi tarehe 14 Shawwal 1434 Hijria sawa na Agosti 22, 2013.
Miaka 386 iliyopita katika siku kama ya leo, vilijiri vita vya mwisho
vya La Rochelle kati ya Wakatoliki na Waprotestanti wa Ufaransa.
Siku kama hii ya leo miaka 315 iliyopita mkataba wa pande tatu kati ya nchi za Russia, Poland na Denmark dhidi ya Sweden ulisainiwa.
Wafalme wa nchi tatu hizo walikuwa na lengo la kuidhibiti Sweden baada ya kumuangusha Sharel wa 12 mfalme kijana wa nchi hiyo. Miaka miwili baadaye mwanzoni mwa mwaka 1700, nchi wanachama wa mkataba huo wa pande tatu ziliishambulia Sweden. Hata hivyo jeshi la Sharel wa 12 liliendesha mapambano na kutoa kipigo kwa nchi hizo vamizi.
Na miaka 153 iliyopita katika siku kama ya hii ya leo Paul Gottlieb Nipkow mmoja wa wavumbuzi wa televisheni alizaliwa huko Ujerumani.
Nipkow alikulia katika familia maskini, lakini juhudi na irada kubwa ilimuwezesha kuendeleza masomo yake ya fizikia hadi chuo kikuu. Paul Gottlieb Nipkow alifanya utafiti mkubwa na hatimaye alifanikiwa kuvumbua transimita ya televisheni. Chombo hicho kilichobuniwa na Nipkow kiliweza kurusha mawimbi ya televisheni katika umbali wa mita 30 na baadaye transimita iliyotengenezwa na mvumbuzi huyo wa Kijerumani ilikamilishwa na wabunifu wengine.
0 comments:
Chapisha Maoni