HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa Fichuo tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Fichuo Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NYOTA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NYOTA. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, Oktoba 20, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE 21/10/2014



MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Wiki hii Mambo yote unayotaka utayapata kwa sharti uache kuwa na wasiwasi na hofu au kupapatika, itakubidi utoe rai nzuri na uache woga na usivunjike moyo unashauriwa kuwaona wazee kwa ushauri zaidi ili kujikinga na mambo hayo.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mchana wa leo patatokea upinzani na undani au maneno yasiyopendeza lakini usiogope. Jihadhari sana kujibizana na watu hasa wale ulio na wasi wasi nao kwamba wanakusaliti. Jiepushe na maneno wiki hote hii.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 21 - DES 21)
Katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo haja yako itatimia. Kuna mtu mkubwa wa hapo unapoisha au kufanyia kazi ndiye atakaye kuonea huruma kwa njia usiyoitegemea. Jiepushe na mambo ya Anasa na Dhambi..

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Ugonjwa au maradhi uliyonayo yataondoka na kupona. Maradhi haya uliyapata au yalitokea kati ya Aprili au Mei au siku yoyote ya Ijumaa au Jumatatu usiku,Wiki hii utapata habari ya mwanamke aliyejifungua mtoto wa kiume.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Unashauriwa kuwa, ukitaka kazi au pesa zizidi lazima uanze tena maana yake ufanye kazi nyingine au kazi yako au biashara uliyonayo uifanye upya, utie vitu vipya na kusafisha na kuitengeneza tena Jaribu kufanya uchunguzi wa mambo kabla hujachukua hatua.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Elewa kwamba wiki hii ni nzuri sana kwako, kuhusu nyumba, au chumba utapata, na harusi uliyopanga kufanya au kuhudhuria pia ipo, lakini kwa sharti ubadili mwendo wako na umuondoe yule anae kupinga kwa kufanya nae urafiki

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Zidisha mapenzi kwa watu wako, fanya sherehe au toa sadaka, yule unaemtaka uwe nae karibu au kama ni kitu basi ukae nacho wewe vinginevyo mambo yako mengi yatakwama na kujikuta ukikosa msaada kutoka kwa watu uliowategemea.

NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Wiki hii yule Mgeni unayemtegemea atakuja, mgeni huyu anafaida aliyoipata au anajishughulisha na mambo ya kazi na atakupa habari ya safari. Safari hiyo ni nzuri.
Unashauriwa kutokata tama upesi kwa kila kitu.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Leo na wiki yote hii zingatia kwamba, kufanikiwa kwa haja zako unazozitaka, lazima uondoe nadhiri uliyoiweka au utimize ahadi fulani ulizoahidi zamani. Elewa kwamba mtu uliekuwa unamtegemea sana atakudanganya na kukuibia bila ya wewe kutegemea. Usimuamini kila mtu hasa wiki hii.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Leo mawazo yako makubwa ni juu ya pesa, maisha na mali. Unataka sana kujua juu ya barua au mtu aliyembali kama atakuja na kama ndoa itatimia na kufanikiwa. Jihadhari sana kufanya mambo kwa pupa hasa shughuli za kikazi au mapenzi. Heshima inaweza Kupotea na utafedheheshwa bila ya kutarajia.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Leo unataka sana kujua kama mtasikilizana na mtu wako wa karibu au kazi mliyoanzisha kama itafanikiwa na kama mgonjwa atapona. Hayo unayoyataka yatakuwa baada ya wiki tatu. Jaribu kuwa mwangalifu na matembezi ya kila siku jioni.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Mchana wa leo ukikutana na mtu yoyote unayemfahamu na akakukimbilia, hiyo ni dalili kwamba kesi yako utashinda na matatizo yako yanayokukabili hivi sasa yataondoka. Pia mtihani utafaulu

Jumanne, Septemba 23, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE 23/9/2014

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo utapata au utapata habari ya mgonjwa. Vile vile kuna habari ya wizi wa pesa, udanganyifu na kuharibika kwa biashara au kazi. Unafikiria sana kukutana na rafiki yako mpenzi, unapenda taabu ya mwanamke au ugonjwa alionao uondoke, unawaza vile vile juu ya ndugu zako namna ya kuwasaidia ili waongoke.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Tatizo lako hivi sasa ni juu ya maneno maneno yaliyotokea kuhusu pesa. Inawezekana ukasimamishwa mbele ya hakimu au mpatanishi. Kazini yako pia tahadhari kuna maneno na watu wengi wanaitaka kazi hiyo. Ndugu yako mwanamke hivi sasa yupo katika taabu. Kuwa muangalifu huenda pia mumeo au mkeo akakuletea taabu.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Siku ya leo ulegevu kidogo tu utakusababishia hasara kubwa usiyoitegemea. mambo yako yanahitaji ujasiri wa hali ya juu kuweza kuyaendeleza

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Hivi sasa una mawazo juu mambo ya mapenzi, mipango ya pesa au kazi. Unapenda leo utembee, ufurahi na usikie muziki lakini kuna ila juu ya mwanamke uanayempenda na ambaye unataka kuwa nae leo..

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo utapata habari ya harusi, tafrija, maulidi, mgeni au barua. Vile vile utasikia habari ya wizi, fitina au mwanamke. Kuna wasiwasi huenda mwanamke au mwanamme unayempenda akakuasi au kutakuwepo na taabu, ugomvi au hiyana kati yenu

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Unafikiria juu ya safari au kupata barua. Inaonekana kuna ushindani au uadui mkubwa juu ya mali au kitu. Una mawazo juu ya mgonjwa unayemuuguza. Vile vile unamfikiria mtoto wako aliye mbali na furaha au ndoa. Unataka sana kupata pesa au kazi.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Mawazo yako ni fikra ya kukutana na wazee au kupeleka barua ya kazi au posa, kupeleka msaada kwa wazee ambao wanaonekana wapo katika taabu na wewe. Hapo ulipou unataka kupata ushindi juu ya vita vinavyokukabili au kama ni ugonjwa basi unataka upone. Ndugu zako pia wana kasoro, rafiki yako mtakutana kwa furaha kubwa sana, haja yako utapata.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Hii leo mchana mambo yako yanaweza kukuendea kombo au kujikuta unakabiliwa na kesi japokuwa utakuja kushinda hapo baadae. Yule adui yako au mpinzani wako aliyekuwa jela atatoka hivi karibuni. Kaa tayari kwa mapambano

NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Leo utapata habari juu ya mtoto, au mpenzi au habari ya pesa ama kazi. kuna kitu fulani kikapotea au pesa kuibiwa au kazi kukutoka. kuna manen au kesi inayohusu mwanamke au kesi hiyo ni ndoa au Talaka..

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Leo una mawazo juu ya safari, mwanamke, bwana au bibi aliyembali na mliopotezana aje au upate habari zake kuna kila dalili kuwa wiki hii utapata raha katika matembezi yako utakayoyafanya hasa muda wa jioni, mpenzi wako atakutembelea na kukuburudisha

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo unafikiria sana mapungufu katika biashara yako au pesa zako. Kuna fitina unafanyiwa katika Kazi. Maisha kwa upande wako yamekuwa yakikutatanisha sana wiki hii Kuna mvutano makubwa na wa hatari katika mapenzi au ndoa kuwa muangalifu sana..

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Jumanne ya leo hakuna muelekeo kwamba matatizo yako yatakwisha au kupungua kwa. mgonjwa uliyekuwa unamuuguza atakufa. Kuna kila Dalili kwamba huko uendako kuna hakuna maelewano yeyote, huyo unayemfuata huko amepanga kukusaliti..

Jumanne, Septemba 16, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMATANO TAREHE 17/9/2014


MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kuna mtu aliye karibu nawe anakusaliti. Ni mtu ambaye unamuamini sana na unafanya naye mambo mengi ya siri, hiyo isikushitue wala kukufanya usitishe shughuli zako. Jambo la kufanya kaa kimya na jaribu, bila ya yeye kujua muondoe katika kazi zako kidogo kidogo.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Jaribu sana leo kuelezea hisia zako kwa watu wako wa karibu, hata kama utajiuma ulimi, wewe sema kilichokuwa katika akili yako, bila woga wala kujali kwamba mtu ataumia au kuudhika kwa maneno yako, au kwamba kwa maneno yako utaharibu mambo.

NGE – SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo kuwa muwazi kwa kila jambo na unatakiwa ujiamini. Haitakushangaza sana kuwa kuna watu wanataka kujiunga na wewe na utamuudhi mtu kwa kumkataa. Elewa kwamba ni vizuri ukawaweka watu hao katika hali ya kukuhitajia zaidi kuliko wao wakikuzoea sana. Kuwa mkali.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo kama ni dereva endesha gari kwa makini kama ni mtembea kwa miguu tahadhari sana. Ikiwa mtu atakukosea adabu aidha barabani au katika matembezi achana nae. Kuna mtoto atataka kuzungumza na wewe mambo ya maana, msikilize. Maneno hayo yanaweza yakawa siyo mazuri kwako lakini mkubalie na msaidie.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Ni wakati mzuri wa kutafakari yale yote uliyosoma au kukutokea mwezi uliopita. Ni wiki ya furaha kwako, wageni watakuja, magomvi yatakwisha na biashara zitafunguka kwa kiasi kikubwa. Usimuudhi mtu wala wewe usikubali kuudhiwa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Hata ukipata ushawishi wa aina gani usikubali kabisa kucheza kamari kwa fedha zako ulizozipata kwa taabu, hata kuziingiza katika biashara yoyote. Ukienda kinyume na maelekezo haya utapoteza pesa au utatapeliwa. Hii ni wiki mbaya kutumia pesa, zihifadhi kuna mazuri yanakuja.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Pamoja na kwamba unajisikia vizuri inakuwia vigumu kukamilisha mipango yako, kuna jambo linakukwamisha katika mipango hiyo. Jaribu sana na usikubali kuwapa watu mawazo yako kwa sababu wengine watakuchezea rafu. Usieleze mipango yako utajikuta umeachwa na wenzio wameitekeleza mbele yako.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Kwa nini kila unayemkabili anakuwa mgumu kwako leo? Inawezekan kwamba wewe ndie unayewalazimisha? Unaweza kuhisi kwamba matakwa yako ni muhimu sana lakini usiwakosee adabu wale unaotaka wakusaidie. Uwe unawafikiria wengine tafadhali.

NG’OMBE – TAURUS (APR 23 – MAY 20)
Nyumbani kwako kuna matatizo au yatatokea matatizo kuna mtu anakupikia jungu. Wewe hupendi mapambano lakini sasa inaonekana uko tayari kupambana. Hiyo ni sawa, kwa sababu kila unapojaribui kuyakwepa mambo yanazidi kuwa makubwa. Pambana nayo sasa uyamalize.

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Ni Nvyema ukaacha vumbi la mkosi uliokupata likatulia kabla ya kufanya jambo lolote jingine.Ni vizuri sana ukifanya mambo kwa faida yako lakini usiwe mbinafsi. Jaribu kutumia njia zote zinazowezekana kukamilisha malengo yako. Kama watu watakasirika usiwajali.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Sayari ya mwezi inaingia katika nyota yako kwa siku kadhaa, hiyo itakupa nafasi ya kupumua. Unachohitajika kufanya ni kutulia kimya na usijiingize katika ugomvi au mabishano ya aina yoyote aidha kazini katika biashara au na wapenzi wako. Huu ni wakati wako mzuri wa kupumzika.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Jumatano hii siyo nzuri kwako hasa katika shughuli za kijamii, usiwe na haraka na jambo lolote, Pumzika nyumbani, lala mapema na tumia muda huo kupanga mipango yako ya wiki inayokuja.

NYOTA YAKO LEO JUMANNE: 16/9/2014

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Mahitaji yako ya leo yatakuwa ni mengi kuliko mapato au kipato chako, jaribu kuyapunguza na ubakie na yale ya muhimu tu ili uweke akiba ambayo itakufaa wewe na familia yako kwa siku za baadae.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Ujumbe ambao umekuwa ukiusubiri wa kukupa idhini ya kufanya jambo fulani utaupata hivi karibuni na utaanza kutekeleza mipango yako kama ulivyotaka, kuwa muangalifu na ufuate maagizo ya wataalam

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ushirika ulionao na watu unaowaita marafiki zako utakutumbukiza mashakani, kwani hao sio wa kuaminika, kuna mambo mabaya na ya haramu ambayo wanayaendesha. Jitege nao kabla hawajakuingiza motoni.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Iwapo kama umepanga kusafiri mahala popote leo hakikisha kwamba unaanza safari mapema kwani kuna uwezekano wa magari kukwama barabarani na kukufanya uchelewe, tegemea siku ya leo kupata shughuli za ghafla na za lazima.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Jihadhari sana na watu utakaokutana nao leo kwa sababu baadhi yao ni wajanja na ukiwategemea wanaweza kukupotosha, ukifaulu kuwaepuka mipango yako ya leo itatimia kulingana na matarajio yako

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kuna jambo ambalo huenda likatokea leo na kugeuza mambo mengine yote ambayo ulikuwa umepanga,hatab hivyo usiwe na khofu kwa sababu litakuwa kwa manufaa yako na washirika wako.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo ni siku nzuri kwako kushughulikia mambo ya familia au jamaa zako ambao umeonekana kuwatupa kwa muda mrefu, Kumbuka kuwa kati ya hao hakuna mwenye kujiweza na kama huwahitaji leo utawahitaji kesho.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Nyota zinaonyesha kuwa kuna bahati itakayokuelekea ya kupata kiasi kizuri cha pesa ambazo unazihitaji sana kwa wakati huu ili kukukwamua kwa mambo yako yaliyokuwa yamekwama, kuwa macho usije ukaipoteza bahati hiyo ambayo pia inahitaji juhudi zako.

NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Leo ni siku ambayo utakuwa na shughuli nyingi za kibinafsi, inaonekana siku nyingi hujasafiri au kupunga upepo, ingawa mwili wako unahitaji sana kupumzika, huu ni wakati bora wa kutenga muda kiasi ili kujipumzisha

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Kuna vikwazo ambavyo vitawekwa katika njia zako za kutafuta riziki na unatakiwa uvitambue na kutafuta njia ya kuviondolea mbali, kuna watu fulani ambao hawafurahii maendeleo yako umepata katika za hivi karibuni na watajaribu kukuangusha.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Kuna uwezekazo kwamba siku ya leo shughuli zako zitakuwa nyingi na zinaweza kukuelemea hata hivyo fanya kadri ya uwezo wako na usije ukahatarisha afya yako, unashauriwa ikiwezekana ulale mapema kwani kazi za kesho pia zinakungojea.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Umekuwa ukihangaika kimya kimya kila unapokumbwa na matatizo ilhali kuna marafiki walio na uwezo wa kukusaidia, Jaribu sana kuweka mambo yako wazi huo usiri uliokuwa nao utakukwamisha

Jumanne, Agosti 05, 2014

NDOTO 10 ZA KAWAIDA NA MAANA ZAKE

It is impossible not to dream. Every single person, all around the world, dream while they are asleep, for minimum 90 minutes. Dreams have always been a topic of mystery among people. Some dreams are straightforward; they are the exact replica of what you are thinking, or were thinking, or of what’s going on in your life. But some dreams are not that easy to decipher. They just do not make sense (for me, that is most of the times). The concept of dreams becomes even more intriguing when it is realized that people across the world have similar dreams. Here are some very common dreams and their meanings.

#1 Falling dream


It is a very common dream. Feeling yourself falling while you are dreaming means that you are trying to hold on to a situation too tightly in your real life, but you don’t have to. If that is so, you should let it go, and let the chips fall where they may.

#2 Flying


If you are flying in your dream, then that means that you have liberated yourself of a thing that has been weighing you down. It also tells us how much control we have over our lives, depending upon how effectively or poorly the flying is handled.

#3 Death


Death is often (for obvious reasons) perceived negatively in the world of dreams. It is often connected with some dramatic change going on in your real life. Symbolically, it represents the end of something in order to start something new.

#4 The naked dream


Most people have the naked dreams only if they feel vulnerable in their real life, be it psychologically, physiologically or emotionally.
 
#5 Being chased


This may be the number one common dream in the world of dreams. It is the most memorable dream, given that it is the most vivid dreams of all. This dream suggests that you are actually running from a situation (or rather say problem) that needs your attention.

#6 Falling teeth


Teeth symbolizes confidence and power. If you dream of your teeth falling out, it means that there is something happening in your waking life that is crushing your confidence.

#7 Unprepared for an exam


Exams are criteria by which we and others generally judge us. If you have a nightmare where you are not prepared for any kind of exam, it means that you are critically examining yourself in your life.
 
#8 Baby


If you are often dreaming of a baby, it doesn’t necessarily mean that you want one. Babies symbolize a start of something new. It could be anything, a project, a new life, et cetera.
 
#9 Being late

 
If you are often late in your dreams (wink!) that indicates that you are losing an important opportunity in your real life, which might be very important to you. It could be because of your busy activity which may or may not be useless.
#10 Vehicles


Vehicles and our control over them represents what path we are taking and how much control we think we have over the path we are taking. If your vehicle is out of your control, it means that we think we don’t have much control over the current situations in our lives.

Jumanne, Julai 29, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMATANO TAREHE 30/7/2014

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Siyo siku nzuri kwako hasa katika shughuli za kijamii, usiwe na haraka na jambo lolote, Pumzika nyumbani, lala mapema na tumia muda huo kupanga mipango yako ya wiki inayokuja.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kuna mtu aliye karibu nawe anakusaliti. Ni mtu ambaye unamuamini sana na unafanya naye mambo mengi ya siri, hiyo isikushitue wala kukufanya usitishe shughuli zako. Jambo la kufanya kaa kimya na jaribu, bila ya yeye kujua muondoe katika kazi zako kidogo kidogo.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Jaribu sana leo kuelezea hisia zako kwa watu wako wa karibu, hata kama utajiuma ulimi, wewe sema kilichokuwa katika akili yako, bila woga wala kujali kwamba mtu ataumia au kuudhika kwa maneno yako, au kwamba kwa maneno yako utaharibu mambo.

NGE – SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo kuwa muwazi kwa kila jambo na unatakiwa ujiamini. Haitakushangaza sana kuwa kuna watu wanataka kujiunga na wewe na utamuudhi mtu kwa kumkataa. Elewa kwamba ni vizuri ukawaweka watu hao katika hali ya kukuhitajia zaidi kuliko wao wakikuzoea sana. Kuwa mkali.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo kama ni dereva endesha gari kwa makini kama ni mtembea kwa miguu tahadhari sana. Ikiwa mtu atakukosea adabu aidha barabani au katika matembezi achana nae. Kuna mtoto atataka kuzungumza na wewe mambo ya maana, msikilize. Maneno hayo yanaweza yakawa siyo mazuri kwako lakini mkubalie na msaidie.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Ni wakati mzuri wa kutafakari yale yote uliyosoma au kukutokea mwezi uliopita. Ni wiki ya furaha kwako, wageni watakuja, magomvi yatakwisha na biashara zitafunguka kwa kiasi kikubwa. Usimuudhi mtu wala wewe usikubali kuudhiwa.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Hata ukipata ushawishi wa aina gani usikubali kabisa kucheza kamari kwa fedha zako ulizozipata kwa taabu, hata kuziingiza katika biashara yoyote. Ukienda kinyume na maelekezo haya utapoteza pesa au utatapeliwa. Hii ni wiki mbaya kutumia pesa, zihifadhi kuna mazuri yanakuja.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Pamoja na kwamba unajisikia vizuri inakuwia vigumu kukamilisha mipango yako, kuna jambo linakukwamisha katika mipango hiyo. Jaribu sana na usikubali kuwapa watu mawazo yako kwa sababu wengine watakuchezea rafu. Usieleze mipango yako utajikuta umeachwa na wenzio wameitekeleza mbele yako.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Kwa nini kila unayemkabili anakuwa mgumu kwako leo? Inawezekan kwamba wewe ndie unayewalazimisha? Unaweza kuhisi kwamba matakwa yako ni muhimu sana lakini usiwakosee adabu wale unaotaka wakusaidie. Uwe unawafikiria wengine tafadhali.

NG’OMBE – TAURUS (APR 23 – MAY 20)
Nyumbani kwako kuna matatizo au yatatokea matatizo kuna mtu anakupikia jungu. Wewe hupendi mapambano lakini sasa inaonekana uko tayari kupambana. Hiyo ni sawa, kwa sababu kila unapojaribui kuyakwepa mambo yanazidi kuwa makubwa. Pambana nayo sasa uyamalize.

Jumatatu, Julai 21, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE 22/07/2014.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Kuna dalili ya kupata ukitakacho, kwanza pana mtu mmoja unayemfahamu ambaye yupo katika shida au ugonjwa unashauriwa msaidie ndio utapata mafanikio. Jaribu kuwa mwangalifu katika matumizi yako, kwani kuna hali ya kukwama huko mbele.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Kuna njama unaundiwa za kukukomoa katika maandalizi yako ya kujiingiza katika mambo ya siasa. Kama pana moto unawaka katika basi lazima uzimwe ili kujisaidia latika malengo yako.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Ukitaka mambo yako yatimie itakubidi uwe mpole na uache fitina. Utapata zawadi kubwa kwa kuwa utafaulu katika mitihani utakayoifanya hivi karibuni. Mpenzi wako yuko njiani anakuja.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Mambo yako mengi unayoyataka yatatimia katika siku za baridi au katika nchi za baridi baridi, au saa za jioni jioni. Kuna mikwaruzano ya hapa na pale itatokea kazini kwako au nyumbani kwako.Unashauriwa usifiche matatizo yako.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Una Matatizo kuhusu wazazi, au uchumba au unyumba, watoto na ukoo wako. Yule mgeni uliyekuwa unamtegemea kuja hivi karibuni atakuja na habari zenye kukufurahisha. Kuhusiana na hayo yanayokusumbua.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Mwezi huu inaonekana unataka uongozi au ukunjufu wa mambo yako unashauriwa kufanya mazoezi kwa bidii nyakati za jioni ili kubadili bahati yako.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mchana huu pana mtu katika nafsi yako unapenda sana kukutana nae na pana jambo ambalo una wasiwasi nalo kama bora ungelifanya au vipi? Huyo mtu haji sasa hivi lakini jambo lako fanya utafanyikiwa.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kwanza lazima ujue kuwa pana mtu wa nyuma yako anakuonea wivu, utapata vikwazo na ugumu wa mambo yako kwa Mchana huu, kuna dalili za kualikwa katika ulevi au wewe kukataa jambo utakaloambiwa na rafiki yako.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Elewa kwamba pana mtu anaejaribu sana kupindua mipango yako na kuiharibu,. Jaribu kupata ushauri na usione taabu kuomba radhi sababu mambo yako yatafunguka.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Huko uendako utagundua siri nyingi ambazo hapo kabla ulikuwa hujazijua na ukitaka kumshinda adui yako ni lazima umfurahie na kumsaidia.Tegemea kupata mwaliko wa kongamano katika siku mbili zijazo.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mipango yako uliyopanga itatimia tu baada ya kuzaa au utakapopata khabari ya mtoto aliezaliwa. Safari yako usiende na Unashauriwa usitembee hovyo hasa ikifikia muda wa jioni. Katika kipindi cha siku tatu.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siri zako zimejulikana na unatakiwa kuwa mwangalifu sana usije ukaumbuka. Ili matatizo yako yafanikiwe itakubidi umpate mtetezi au wakili na usione haya kutaka msamaha na kumsifu anae husika.

Alhamisi, Julai 17, 2014

NYOTA YAKO LEO JULAI 17

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Leo Karibisha wageni, fanya vitendo vizuri saidia sana haja za watu
na itakufanya ufanikiwe katika mipango yako au matibabu yako au ya jamaa yako aliyeugua kwa muda mrefu.. Mgonjwa akipona toa sadaka.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Hivi karibuni kuna mtu unaetaka kukutana nae lazima mtakutana lakini itakubidi umfuate,na uzungumze naye, kwani hakuna la maana utakalolipata usipomfuata. Mipango itatimia tu baada ya kukutana nae.
MASHUKE – VIRGO(AUG 24- SEPT 23)
Kuna Mtu atakuja leo kukusaidia, akija mwinukie, atakuwa anatoka upande wa Magharibi au Kusini na atakuja muda wa jioni, Jihadhari kuna mikakati mibaya inaundwa juu yako, unashauriwa kuhama mji au kubadili kazi yako ya sasa
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Mchana huu kuna mtu utakutana nae, mtu huyo anaweza kuwa mpenzi, anaweza kuwa mpenzi au mtu mtakaesikilizana sana. Mpokee na kuwa nae utafanikiwa na atakuinua sana kimaisha. Kuna habari za sherehe utapokea katika kipindi cha siku mbili.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Kama leo mchana kama unamipango na mtu yoyote usione shaka kumkabili, mwelezee na mambo yako yatafunguka japokuwa yatakuwa na hasara kubwa na faida kidogo usikate tamaa huo ni mwanzo tu, baadaye mambo yako yatakuwa mazuri sana.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Wiki hii kuna dalili ya kutokea matokeo ya kutatanisha au kupotelewa na vitu vyako kiajabuajabu. Utapata habari ya kifo na Unaweza uchanganyikiwe. Unashauriwa kuwa mvumilivu kwani kifo hiki ndio ufunguo wa bahati yako.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo usione tatizo kumtolea mtu wako wa karibu shida zako utapata haja yako mara moja kama si leo, Jumatatu au Mwezi wa Septemba lakini itatimia.
Elewa kuwa mfanyakazi wako wa ndani au msaidizi wako katika kazi au biashara amegundua siri zako na ana mpango wa kuzitangaza. Muwahi kabla hujadhurika.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kuna wasiwasi kuwa utapata maradhi ya kifua ambayo yatakusumbua sana lakini mwishowe utapona kwa msaada wa rafiki yako.Jaribu kuwa nyumbani nyakati za jioni jiepushe na safari za usiku kuepukana na upepo mbaya utakaokuingia kifuani.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Pana mtu anaitwa Yusufu au Joseph au jina lake linaanza na mojawapo ya herufi zilizo katika majina hayo atakusaidia na lazima ushirikiane nae.mtafute na utapata faida kubwa.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo kama kuna mtu unayetaka kushirikiana nae jina lake linaanza na moja ya herufi hizi ‘ ‘S’, ‘F’, ‘P’, ni vizuri zaidi.Mtu huyo atakusaidia kugundua njama unazofanyiwa na jamaa zako wa karibu, unashauriwa kujifanya kama hujazijua njama zao ili kuzipata za ndani zaidi.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mchana huu Pendelea sana kumsifu kila utakae kutana nae utaona ajabu. kwamba mambo yako yatanyooka na kufanikiwa kwa hali ya juu sana, unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa sadaka.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mchana huu una mawazo sana kuhusu Ndoa au Mwanamke au Mwanamme. Mambvo hayo yatafunguka baada ya siku saba . Unatahadharishwa usijishughulishe na ugomvi wowote utakatokea hapa mtaani kwako hata kama ni mtoto wa jirani yako, kwani kujiingiza kwenye ugomvi huo ni kujitakia balaa kubwa.

Jumatatu, Julai 14, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE 15/7/2014

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Elewa kwamba huyo unayemfuata huko unakokwenda amepanga kukudanganya, ni vyema usiende. Wiki hii ukimwona mtoto amelala kwenye godoro nje ya nyumba, basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna ugomvi unakuja na kutakuwa hakuna maelewano yeyote mtakayoyafikia,

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Matatizo yako ya kifedha yaliyokuwa yanakuandama wewe mwenyewe au familia yako yatakwisha.Kuna mpango utaletewa ambao utakukwamua katika ukwasi. Na ikiwa wiki hii utakutana na mwanamme kabeba Ndoo, hiyo ni dalili kwamba matatizo yako yatakwisha kabisa.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo mambo yako mengi yatakuwa hadharani, yatakufedhehesha na kukuaibisha sana, unashauriwa kuwa makini na kila unalotaka kulifanya. Na ikitokea ukimuona mtu ameshika Panga, hiyo ni dalili kwamba utaaibika

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo ukikutana na mtu ambaye Sharubu mchanganyiko nyingi basi ujue kuwa mambo yako utakayo yafanya kwa ushauri wa rafiki yako yatakuwa mabaya, Elewa rafiki huyo ni adui na hatakusaidia .Jiepushe naye.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako yanahitaji ujasiri wa hali ya juu kuweza kuyaendeleza, ulegevu kidogo tu utakusababishia hasara kubwa usiyoitegemea. Jaribu kuwa mkali na ufatilie kwa karibu mipango yako yote.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo hii katika shughuli zako za kawaida ukikutana na Mlevi, hiyo ni dalili kwamba kuna safari ya mbali na yenye faida itakujia. Ukipata nafasi hiyo usiiachie.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mambo utakayoambiwa Leo hii yatakuwa ya kweli Hakikisha kila neno unaloambiwa unalifanyia kazi hasa masuala yanayohusiana na mapenzi na biashara. Usiyapuuzie hata kidogo

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Leo kuna kila dalili kuwa mambo yako yatafunguka na mikwamo ya hapa na pale itapotea, baada ya muda hali itaendelea kuwa nzuri na matatizo yaliyokujia kwa kasi yatapotea na kukuacha ukiwa na furaha

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo mipango yako itakuwa mizuri. Epuka kupingana pingana na watu unaofanya nao Biashara, Jihadhari na marafiki zako inaonekana wiki hii watakujia na mpango ambayo usipokuwa makini itakupotezea pesa.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Leo kuna dalili ya mambo yako kukuendea vizuri lakini utajikuta unakabiliwa na kesi ijapokuwa kesi hiyo utakuja kushinda hapo baadae. Yule rafiki yako au ndugu yako aliyekuwa jela atatoka hivi karibuni, lakini atakuletea matatizo makubwa.

NG’OMBE – TAURUS (APR 23 – MAY 20)
Leo huko uendako utakumbana mambo ya kufurahisha au kutatokea hali ya makubaliano na mtu uliyemkopa.Unashsuriwa baada ya matatizo haya usijaribu kukopa tena wuiki hii unaweza kushiondwa kulipa.

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Wiki hii yule adui yako atakutembelea na kukuudhi.naikitokea ukikutana na mtu mzigo wa aina yeyote, basi elewa kuwa utaona mambo ya ajabu katika matembezi yako utakayoyafanya jioni ya kesho,

Alhamisi, Julai 10, 2014

NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI: 10/7/2014


KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Elewa kuwa kuna mpinzani wako wa karibu asiyependa maendeleo yako. Anajaribu kila njia kukutafutia mabalaa.Unashauriwa ili kuepukana na hayo ni vyema ukahama sehemu uliyopo hivi sasa.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Mambo yako uliyoyapanga ili kupata pesa siku ya leo yatasimama au kuwekewa vikwazo vya hapa na pale. Na watakaofanya hivyo ni watu wako unaowaamini. Jaribu kuachana na mipango hiyo mpaka baadae.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku ya leo jitahidi sana kujibidiisha na kufuatilia mipango yako. Mambo yako yote uliyopanga yako tayari isipokuwa kuna mtu anayashilikia. Jaribu kuzungumza nae hata kama ikiwa ni kutoa kitu kidogo ili yawe sawa, wewe toa. Faida ni kubwa kuliko hasara

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Kuna mpenzi wako alie mbali na wewe unamkufikiria sana. Elewa kuwa mpenzi huyo yupo njiani anakuja kukutembelea na kukuletea msaada.Jaribu kuweka mambo yako sawa ili akija akute kila kitu kizuri. Utapata faida kubwa kwake.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Usipokuwa muangalifu katika siku mbili hizi kuna dalili ya kumpoteza mpenzi wako wa muda mrefu, Inaonekana pia kuna dalili ya kupoteza kitu chako cha thamani sana, chunga sana hali ya kusahausahau.Weka vitu vyako vizuri

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo katika matembezi yako ukikutana na mtu amebeba Samaki, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yatafunguka, Lakini unatakiwa kuwa makini sana na watu watakaokujia na kutaka msaada kwako, kila samaki mmoja utakayemuona ni Bahati moja nzuri.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo kuwa muangalifu sana unaweza kuletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha. Biashara yoyote kwa leo haifai. Kuhusu kazini kuna mtu anakuchimba anataka ufutwe kazi jaribu kufanya mambo yako kwa makini hasa kazini.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Usiwe muoga kutoa msadaa kwa matatizo yanayowapata wenzio hasa kama mkiwa mmeongozana pamoja. Jaribu kurekebisha hiyo tabia yako ya ubahili mara moja vingenevyo itakuleta balaa.uktakapotoa ndio utakavyopata.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kuna dalili kwamba mpenzi wako atakughasi kwa maneno maneno kila wakati kuhusiana na uhusiano wako nje ya ndoa. hata kama wewe utakanusha lakini yeye bado atashikilia msimamo wake kwani amepewa habari za uhakika. Jaribu kuwa mpole ili balaa liishe..

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo Kuna dalili za kuletewa zawadi kutoka kwa rafiki yako. Zawadi hizo zitakufariji sana. Ile migogoro yako katika mapenzi haitakwisha hivi karibuni na kama ulikuwa unaugua au unauguza mgonjwa basi utachelewa kupona na mgonjwa wako hatapata nafuu haraka.

NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Ile biashara unayotaka kuifanya na uliipanga wiki hii itakuletea faida kubwa ambayo itakusaidia katika mipango yako ya baadae. Yale makosa yako na madhambi uliyomfanyia rafiki yako au utasamehewa Jaribu kuwa muangalifu.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Ile mikosi inayokuandama nyumbani na kazini itaendelea tena wiki hii. Ili Kuondoa hali hiyo pata msaada kutoka kwa watalaamu wakusafishie nyota yako, vinginevyo mambo yako yatakuwa mabaya zaidi.

Jumatatu, Juni 30, 2014

NYOTA ZENU LEO JUMANNE 1/7/2014


KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku yoyote wiki hii utapatwa na balaa la kupigwa bila ya kutegemea na bila kosa lolote na hata kama lipo kosa basi kosa hilo hukulifanya wewe Matatizo yako yatachelewa kumalizika kwa hiyo lazima usubiri huenda pakatokea matatizo ya kufungwa au kuharibikiwa vibaya.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo kuwa na tabia ya ukaidi na utundu, tumia akili nyingi busara na uwe mwepesi kuelewa mambo.Yale tu utakayoyafanya wewe mwenyewe ndiyo yatakayofanikiwa, lakini yale yote utakayoyaagiza yafanywe na watu wengine yatalala.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo jaribu kuwa na tabia ya kuwa na Matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea, maendeleo yako yatakuwa ni madogo na yatakuwa yanaenda polepole sana. Biashara yako pia itapanuka kwa kusuasua.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo jitahidi kuwa na uhuru wa kupenda kuchagua. Fanya mambo kwa ukamilifu na usipende mambo nusu nusu. kama kwako kuna au unamfahamu mjamzito basi elewa kwamba atazaliwa mtoto wa kike, kabla ya siku saba

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo kuwa thabiti usipende kuharakishwa katika mambo yako na kuwa mtulivu na uwe na tabia ya uaminifu na Uadilifu. Usimamizi wa karibu unahitajika kwa kila jambo unalotaka kulifanya. Unashauriwa kuwa makini na kila unachotaka kukifanya, ,

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Mchana wa leo kuna habari za uongo utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana ndugu zako Jaribu kufanya uchunguzi kabla hujachukua hatua. usipende kuamrishwa na watu wasioweza kutii amri zako.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Ili kupata mafanikio wiki hii kuwa tabia ya kutekeleza wajibu wako ipasavyo. Fanya w bidii katika kazi, kuwa muaminifu, mstahamilivu, na uwe na tamaa ya cheo na hali bora kimaisha. Usiwe na tabia ya uchoyo na ubinafsi utakwama.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Mchana wa leo utapata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha. Tenda wema kwa watu na usiwe na tabia ya kufanya vitu kwa ghafla bila kufikiria. Wiki hii utapata marafiki wengi.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku hii ya leo acha tabia ya kutoshawishiwa na maneno ya watu. punguza ubinafsi na kujipendelea sana. usiwe dhaifu na goigoi. Ukifanya hayoutapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa madhambi uliyomfanyia rafiki yako.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
siku ya leo kuwa mvumilivu kwa jambo lolote, usiwe tabia ya kujitoa muhanga. vinginevyo mambo yako yataenda kombo, Unashauriwa kuwa mtulivu na hali hiyo kwa kuwa ni hali ya muda mfupi tu.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo hii punguza mawazo na usiwe na tabia ya kufikiria mambo mengi kwa wakati mmoja ambayo hayatekelezeki. Elewa kwamba watu hawakuelewi vizuri. Kuna mambo mengi ambayo ulikuwa umefichwa kwa muda mrefu na watu wako wa karibu. Ili kuleta baraka leo nenda kawatembelee wazee wako.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Hivi sasa kuna watu wanaokutia nguvu na kujifanya kukusaidia ni wapenzi wako kwa nje tu lakini kwa ndani wao ni maadui zako epukana nao. Epukana nao na fanya mambo yako bila kuwashirikisha.

Jumanne, Juni 24, 2014

NIMEIPENDA HII 'NAMNA YA KUPATA KITU KILICHOIBIWA AU KUPOTEA'

Katika nyota na elimu ya Nambari (Numerology) kuna njia ya kuweza kukufanya uweze kugundua kilichoibiwa au kupotea au ambacho umekiweka mahala na huwezi kukumbuka ni wapi.

Njia ya kufanya ni kama ifuatavyo:

1. Unapopoteza kitu unatakiwa kwanza utulie usipate hofu wala kubabaika.

2. Unatakiwa utulize mawazo yako na uanze kukifikiria hicho ulichokipoteza.

3. Unatakiwa uandike kwenye karatasi nambari tatu kati ya 1-9 ambazo zitakuja katika akili yako kwa wakati huo.

4. Jumlisha namba hizo upate nambari moja.

Mfano: umeandika namba 4, 5, 2 unajumlisha 4 +5 + 2 = 11 unaendelea

1 + 1 = 2.

Majibu ni kama ifuatavyo:

KAMA IKIBAKI 1:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kusini hasa katika sehemu muhimu ya nyumba yako, Sebuleni au Chumbani.

• Kiko karibu na pazia nyeupe au shuka nyeupe au nguo nyeupe katika sehemu tulizozitaja.

• Kama hukioni kitu hicho muulize mtoto aliyepo ndani ya nyumba yako atakuonyesha.

KAMA IKIBAKI 2:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kusini hasa karibu na Karo au Beseni au sehemu mnayotumia kwa kufua nguo.

• Kitu hicho utakipata kwa msaada wa Mtu hasa Mwanamke anayeishi hapo kwako.

• Angalia sana sehemu ya kwenye tanki la maji au sehemu maji yanapopita au karibu na nguo zilizofuliwa.

KAMA IKIBAKI 3:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kaskazini ndani ya makaratasi au vitabu au makabrasha yako au ukumbini.

• Umekipoteza katika sehemu ambayo ulikuwa ukifanyia kazi au ofisini au karibu na boksi au magazeti

• Angalia ndani ya Boksi au kwenye kabati la vitabu au katika kitu ambacho kinajifunga mara mbili kama faili au muulize mtoto.

KAMA IKIBAKI 4:

• Kitu hicho unacho mwenyewe lakini umesahau.

• Kiko upande wa Kaskazini angalia kwenye Rafu (Shelf) utakikuta hapo

• Kama hukioni angalia kwenye kabati la nguo au sehemu unapoweka tai zako au mikanda.

KAMA IKIBAKI 5:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana kwa urahisi upande wa Magharibi. Hasa sehemu unazoweka kofia vilemba au kitunga.

• Jaribu kutafuta sehemu unazoekea nguo.

• Kitu kiko katika shubaka au kwenye kitu msatili au sehemu unayowekea viatu.

KAMA IKIBAKI 6:

• Kitu hicho itakuwa vigumu kukipata, lakini angalia upande wa mwisho Mashariki au Magharibi, sehemu ambayo kuna viatu au malapa.

• Jaribu kuangalia kwenye kitanda au kwenye stendi ya vitu au kwenye rafu (Shelf).

• Kama hukioni muulize Mumeo au Mkeo, kitakuwa katika vitu vyako vya binafsi.

KAMA IKIBAKI 7:

• Kuna uwezekano usikipate kitu hicho lakini jaribu kuangalia upande wa Mashariki katika kitu cheupe kama ni nguo au shuka au karatasi jeupe kiangalie utakiona hapo.

• Kuna uwezekano wa kudanganywa au watu wako kukataa kukupa taarifa kuhusu kupotea kwa kitu chako.

KAMA IKIBAKI 8:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Kaskazini hasa katika sehemu tambarare au jaribu ndani ya kabati.

• Kiko karibu na sehemu unapoweka vitu vyako vya thamani kama fedha na dhahabu.

• Ukianza kukitafuta angalia chini ya mguu wako utakiona.

KAMA IKIBAKI 9:

• Kitu hicho kinaweza kupatikana upande wa Mashariki hasa katika sehemu ambayo kuna nguo za watoto.

• Tia mkono wako kwenye nguo na papasa papasa utakiona.

• Kitu kilichopotea kiko ndani ya familia, Kama hukioni kiangalie kwenye chumba cha watoto au kwenye vitu vya zamani au kwenye sehemu yenye giza au kwenye kona.

MAANA YA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA YENU


A; Haraka, Pupa ya Maisha
Wenye jina linaloanza na herufi ”A” ni Watu wanaopenda mambo makubwa, Wanajiamini, na wenye uwezo wa kutimiza malengo yao, Ni watu wenye tahadhari Katika kila jambo, Wachangamfu na wanaopenda Matukio. Wanapenda kuheshimiwa, Wanapenda mamlaka, Wana kiburi na ni Watu wenye hasira.

B; Inawakilisha Kazi, Pesa, Mapenzi, Ujenzi.
Wenye jina linaloanza na herufi “B” ni Watu Wakarimu , Waaminifu na Wenye kupenda kazi. Ni watu Jasiri, Shujaa na Wakatili katika vita au pale wanapotaka kulinda vyake au vilivyo katika himaya au Mamlaka yao.

C; Inawakilisha Vurugu, Ndugu, Kuchanganyikiwa.
Wenye jina linaloanza na herufi “C” ni Watu wa kubadilika badilika, Washindani, na hupenda kupigania Malengo yao wanayoyapenda. Ni watu Wabunifu, na wanaopenda Mawasiliano.

D; Inawakilisha Upole, Kuchelewa, Wazee, Cheo.
Wenye jina linaloanza na herufi “D” ni Watu wanaopenda Usawa, na Kufanya Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na wenye kupenda Usafi. Ni jeuri na wenye Msimamo.

E; Inawakilisha Kisomo, Maendeleo, Watoto.
Wenye jina linaloanza na herufi “E” ni Watu wenye roho nzuri, Wenye mapenzi, wenye huruma, wenye kupenda uhuru katika mapenzi na wachangamfu sana. Kinyume na hivyo ni watu wasiotegemewa na vigeugeu.

F; Inawakilisha Kusahau, kupoteza,Kusoma mbali.
Mwenye jina linaloanza na herufi “F” ni Watu wenye mapenzi, huruma, Roho nzuri na Uwezo wa kuwafariji watu. Ni Watetezi wa Watu na wenye huzuni na hisia kali wanapoudhiwa, Lakini ni wazito sana kufanya maamuzi ya haraka.

G; Inawakilisha Ndoa, kuunganisha,Mikutano, kufuzu Baada ya Ndoa.
Mwenye jina linaloanza na herufi “G” ni Watu wenye Imani ya kidini na nguvu za kiroho, Wana Vipaji vya kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni watu wenye hisia kali, Wanaopenda kusoma au kujiendeleza, wakati mwingine wapenda upweke, na wakaidi kukubali ushauri wa watu wengine.

H; Inawakilisha kupoteza, kupata tena,Mafanikio, kutumia nguvu au kesi au vurugu.
Wenye jina linaloanza na herufi “H” ni Watu wenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na nguvu zao binafsi, ni watu wanaojituma sana. wenye mawazo na fikra nyingi mengi lakini wana udhaifu wa kuwa wachoyo na wabinafsi.

I; Inawakilisha kubadilisha, kubadilika,kusafiri, Ugenini.
Wenye jina linaloanza na herufi “I” ni Watu wenye kupenda Sheria na Mpangilio, wana Huruma na Utu. Ni Viumbe ambao wanajiamini sana katika mambo yao lakini wana hasira za Haraka Haraka.

J; Inawakilisha kuongoza, Siasa,Biashara, Ukubwa.
Wenye jina linaloanza na herufi “J” ni Watu Wenye matamanio, Wakweli, Wakarimu, Waerevu na Wajanja, Wasiokubali Kushindwa na kutokana na tabia yao hiyo Hupata mafanikio Makubwa. Kasoro yao ni kwamba kuna wakati wanakuwa wavivu na waliokosa mwelekeo.

K; Inawakilisha kufuzu, kupitia,rafiki, kuungana.
Wenye jina linaloanza na herufi “K” ni Watu wenye Ujeuri, wenye msimamo thabiti, Mashuhuri na wenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za Watu, wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengine hawana. Ni watu wasioridhika na hali ya kimaisha.

L; Inawakilisha kupingwa, kupingana,mafanikio baada ya shida na Safari.
Wenye jina linaloanza na herufi “L” ni Watu wa Vitendo, wenye hisani na wanaopenda kujipanga vizuri kimaisha, wajihadhari na ajali za mara kwa mara kubwa na ndogo.

M; Inawakilisha Mabadiliko baada ya kurejea au baada ya Talaka.
Wenye jina linaloanza na herufi “M” ni Watu Wenye kujiamini sana, wachapa kazi na hupata mafanikio, Ni watu waropokaji, wenye haraka na wepesi sana kukasirika.

N; Inawakilisha kukwama kipesa,mafanikio baada ya kurejea kazini au nyumbani.
Wenye jina linaloanza na herufi “N” ni Watu wenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana, kasoro yao kubwa ni kwamba wana wivu sana.

O; Inawakilisha Uzazi wa watoto, kuleta bahati, Ushindi kimchezo au kimasomo.
Wenye jina linaloanza na herufi “O” ni Watu wenye subira, wavumilivu na wenye bidii ya kusoma. Ni watu wenye kupenda kutumikia jamii na wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

P; Inawakilisha kupotelewa, Kuuguliwa, Wizi na Masomo ya Juu.
Wenye jina linaloanza na herufi “P” ni Watu wenye Uwezo wa kuamrisha na Hekima Kubwa. Wana nguvu za kiroho lakini wanapenda sana kujitumbukiza katika mambo ya watu.

Q; Inawakilisha Ndoa, kufuzu baada ya kurejeana
Wenye jina linaloanza na herufi “Q” ni Watu wenye kupenda mambo ya asili, Ni watu wasiolezeka au kutambulika tabia zao kirahisi na wana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana, hata hivyo ni watu walioopooza sana.

R; Inawakilisha Kuporomoka na kupata nguvu, kusafiri mbali na kushinda.
Wenye jina linaloanza na herufi “R” ni Watu wenye Uvumilivu, wenye huruma lakini wana hasira za haraka, muda wote wanakuwa ni watu wanaopenda Amani na hawataki ugomvi.

S; Inawakilisha kufuzu Ugenini, Kupata mali na Magari.
Wenye jina linaloanza na herufi “S” ni Watu wenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya Ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

T; Inawakilisha Kupata Utajiri na kujenga, Kesi, baadae kushinda
Wenye jina linaloanza na herufi “T” ni Watu wenye kupenda ushauri wa kiroho, wanatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na wepesi kushawishika.

U; Inawakilisha Ushindi wa Pesa, Kunyanganywa mali na Kesi za mara kwa mara.
Wenye jina linaloanza na herufi “U” ni Watu wenye bahati kubwa kwa ujumla, wanapenda uhuru katika mapenzi, lakini ni wabinafsi wenye tamaa na waliokosa maamuzi

V; Inawakilisha Utajiri wa Bahati Nasibu, kupewa, kuokota na ndoa nyingi.
Wenye jina linaloanza na herufi “V” ni Watu wachapa kazi wenye bidii na wasiochoka, hata hivyo ni watu wasiotabirika.

W; Inawakilisha, Pesa, Kazi, ni rahisi kusaidia watoto wengi.
Wenye jina linaloanza na herufi “W” ni Watu wawazi na wachangamfu kupita kiasi na wenye uwezo wa kumtambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye Tamaa na hufanya mambo ya hatari.

X; Inawakilisha Kupata uzazi, Kupata jengo na Utajiri
Wenye jina linaloanza na herufi “X” ni Watu wasiopenda kuwekewa vipingamizi katika mambo yao, wanapenda anasa na ni rahisi kujiingiza katika mambo yasiyofaa na kujitoa uaminifu.

Y; Inawakilisha Kupata Bahati, Uandishi, Watoto na Uongozi.
Wenye jina linaloanza na herufi “Y” ni Watu wenye kupenda uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na huwasababishia wao kupoteza bahati zao katika maisha.

Z; Inawakilisha kuuguliwa Watoto, vitu kupotea, Shida za Pesa na Kazi.
Wenye jina linaloanza na herufi “Z” ni Watu wenye kupenda matumaini na Amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.

Jumanne, Juni 17, 2014

NYOTA ZENU LEO 17/6/2014



MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Hivi sasa kuna watu wanaokutia nguvu na kujifanya kukusaidia ni wapenzi wako kwa nje tu lakini kwa ndani wao ni maadui zako epukana nao. Epukana nao na fanya mambo yako bila kuwashirikisha.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku yoyote wiki hii utapatwa na balaa la kupigwa bila ya kutegemea na bila kosa lolote na hata kama lipo kosa basi kosa hilo hukulifanya wewe Matatizo yako yatachelewa kumalizika kwa hiyo lazima usubiri huenda pakatokea matatizo ya kufungwa au kuharibikiwa vibaya.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo kuwa na tabia ya ukaidi na utundu, tumia akili nyingi busara na uwe mwepesi kuelewa mambo.Yale tu utakayoyafanya wewe mwenyewe ndiyo yatakayofanikiwa, lakini yale yote utakayoyaagiza yafanywe na watu wengine yatalala.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo jaribu kuwa na tabia ya kuwa na Matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea, maendeleo yako yatakuwa ni madogo na yatakuwa yanaenda polepole sana. Biashara yako pia itapanuka kwa kusuasua.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo jitahidi kuwa na uhuru wa kupenda kuchagua. Fanya mambo kwa ukamilifu na usipende mambo nusu nusu. kama kwako kuna au unamfahamu mjamzito basi elewa kwamba atazaliwa mtoto wa kike, kabla ya siku saba

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo kuwa thabiti usipende kuharakishwa katika mambo yako na kuwa mtulivu na uwe na tabia ya uaminifu na Uadilifu. Usimamizi wa karibu unahitajika kwa kila jambo unalotaka kulifanya. Unashauriwa kuwa makini na kila unachotaka kukifanya, ,

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Mchana wa leo kuna habari za uongo utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana ndugu zako Jaribu kufanya uchunguzi kabla hujachukua hatua. usipende kuamrishwa na watu wasioweza kutii amri zako.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Ili kupata mafanikio wiki hii kuwa tabia ya kutekeleza wajibu wako ipasavyo. Fanya w bidii katika kazi, kuwa muaminifu, mstahamilivu, na uwe na tamaa ya cheo na hali bora kimaisha. Usiwe na tabia ya uchoyo na ubinafsi utakwama.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Mchana wa leo utapata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha. Tenda wema kwa watu na usiwe na tabia ya kufanya vitu kwa ghafla bila kufikiria. Wiki hii utapata marafiki wengi.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku hii ya leo acha tabia ya kutoshawishiwa na maneno ya watu. punguza ubinafsi na kujipendelea sana. usiwe dhaifu na goigoi. Ukifanya hayoutapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa madhambi uliyomfanyia rafiki yako.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
siku ya leo kuwa mvumilivu kwa jambo lolote, usiwe tabia ya kujitoa muhanga. vinginevyo mambo yako yataenda kombo, Unashauriwa kuwa mtulivu na hali hiyo kwa kuwa ni hali ya muda mfupi tu.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo hii punguza mawazo na usiwe na tabia ya kufikiria mambo mengi kwa wakati mmoja ambayo hayatekelezeki. Elewa kwamba watu hawakuelewi vizuri. Kuna mambo mengi ambayo ulikuwa umefichwa kwa muda mrefu na watu wako wa karibu. Ili kuleta baraka leo nenda kawatembelee wazee wako.

Jumatatu, Juni 02, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE: 03/6/2014

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo una shughuli nyingi sana za kufanya na hiyo kazi unayoifanya inahitaji nguvu bidii na akili kuikamilisha. Unatakiwa ujikakamue ili uweze kuikamilisha vinginevyo utapata matatizo.washirika wako watakufurahia ukiikamilisha. Ni vyema ukamshirikisha huyo unayemfikiria kwa sasa.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Jambo lolote lililokuwa linakutia wasiwasi hapo awali, ikiwa ni masuala ya fedha, mambo ya hisia au kazi suluhisho litakujia kiajabu ajabu. Utagundua ghafla njia ya kukufanya uondokane na matatizo hayo na itafanyika bila ya kumuudhi yoyote. Wote wanaokuchukia watafurahi.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Bado mawimbi ya wasiwasi yanakuandama lakini kwa vile sasa ule uzito umepungua umepumzika kidogo na watu wanakufurahia sana, Jaribu kukaa nyumbani, pumzika na tafuta ushauri. Hakuna njia nyingine.

MASHUKE – VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama ikiwa kazi zako zinahusisha watoto au ukiwa una watoto wako mwenyewe, jihadhari na tabia yako mbaya. Mmoja wa watoto hao anaweza kukuumbua kwa kutoa siri zako kwa watu. Hiyo inaweza kukuletea balaa.

MIZANI – LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo utapata furaha ya kukutana na rafiki yako wa zamani au mshirika wako. Kama akikutaka akununulie chai au kahawa au chakula nenda wala usisite kwa sababu kuna habari atakupa na zitakusaidia sana kukubadilisha kimaisha.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo unaweza kusamehewa iwapo utakuwa inajisikia vibaya na huwezi kutekeleza majukumu yako,kuwa mkarimu kwako mwenyewe na kwa watu wengine na usifanye jambo lolote ambalo hulipendi, na kwa kufanya hivyo hata ikibidi ujifungie chumbani kitandani kwako fanya hivyo.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
.Usikubali mtu yoyote akuchokoze, umeshaelezea hisia zako na umeshawasikiliza watu hisia zao. Kuna watu wanataka kupambana na wewe lakini wewe unajihisi kwamba una amani ndani ya moyo wako. Shirikiana na marafiki zako walio karibu leo jioni.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
wapenzi watakujia kwa wingi wiki hii, na katika hao utaweza kupata mmoja ambaye utakuwa nae kwa muda mrefu. Hao wengine unaweza ukafurahi nao kwa muda. Kati ya hao kuna wengine pamoja na kukutaka urafiki watakuwa sio wazuri.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 28)
Kipindi hiki inaonekana matatizo yameshaanza kukuandama, inaonekana unaanza kuchanganyikiwa kutokana na mzigo wa matatizo ulionao. Unajua kabisa kwamba kuna majukumu ambayo unatakiwa uyatekeleze lakini hujayafanyia kazi. Unashauriwa kwamba yatekeleze hayo majukumu haraka sana itakusaidia kuondokana na shida.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kuna mambo ambayo yanakushinda kuyaingia na kuyatekeleza, fanya subira utagundua mengi yaliyofichika katika hayo.ikiwezekana jaribu kuyaacha na uwe mtulivu kuna mengi mazuri yako njiani yanakuja.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Kuwa muangalifu sana iwapo mtu yoyote atataka umshauri katika jambo lolote. Unaweza ukawa mtego ambao utakutumbukiza katika matatizo. Kwa hivi sasa jitahidi kujiepusha na kujiingiza katika jambo lolote na utafute njia ya kujitoa iwapo umo katika mpango au mradi hasa wa kifedha.

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Wiki hii utapata kazi au mpango mzuri wa kifedha ambao utakukwamua kutokana na matatzizo ya ghafla yaliyokufika. Mtafute rafiki yako mpendwa na mpelekee kilio chako, atakusikiliza na kukusaidia. Mamb yako karibu kufunguka kuliko unavyofikiria

Alhamisi, Mei 08, 2014

NYOTA YAKO LEO IJUMAA TAREHE 9/05/2014

NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Siku tatu zijazo utapata mafanikio katika mambo yako unayotegemea kuyafanya, dalili utaziona iwapo utakwenda mahala popote na ukafuatwa na mtoto wa kiume, unashauriwa kuongeza bidii na ubora wa kazi zako ili kupata mafanikio.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Kati ya siku ya leo na jumapili zitakuwa siku ya furaha kwako, mipango yako yote uliyotarajia itakamilika, mgeni unayemtegemea yuko njiani na mpenzi aliyekutoroka atarudi. Mipango yako hakikisha unaifanya katika kipindi cha masaa 24 kuanzia sasa.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Wikiendi hii utapata habari ya mgonjwa au wewe mwenyewe utauguwa, ikikutokea mchana huu katika matembezi yako ukakuta mbwa anakula mfupa inaashiria kuharibika kwa mambo yako.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Yule umpendae atakujia na kushirikiana na wewe kwa kila utakalomuomba kulifanya bila ya kipingamizi chochote. Pia utaona mambo ambayo yatakufurahisha sana hasa nyakati za jioni au usku.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo kuna mambo mengi utayaona ya kukufurahisha na kukupendeza, masuala ya mapenzi yatakufurahisha zaidi kipindi hiki. Unashauriwa ujivunie utakayoyaona leo wala usiseme kitu

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Wiki hii kuna kila dalili ya kupata pesa. Jitahidi kufanya mipango yako yote na uwaendee unaowadai na utapata ukitakacho.pesa ukipata zitumie katima mambo uliyopanga usibadilishe.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo kuna kila dalili ya kupata marafiki wazuri.Mchana ikitokea ukikutana na mtoto mdogo mwenye sura mbaya basi ujue hiyo ni ishara ya kwamba marafiki zako wanakufanyia hila na watakusalilti katika biashara yenu

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Mambo yako mengi yaliyofungika yatafunguka ghafla. Na ukikutana na watoto wengi pamoja, hiyo ni ishara ya kwamba utaridhika na mambo yanayofanyika. Kuna barua ya kusikitisha utaipata wiki hii.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Wiki hii kutatokea mabadiliko ya ghafla kazini kwako lakini kwa manufaa yako, lakini ukiona Mchwa popote wameingia ndani ya nyumba, hiyo ni ishara ya kwamba utapata kazi na utakuwa wakati mgumu mbele yako.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo hii kuna kila dalili ya kupata mkosi na kuvurugika kwa mambo yako, kila jambo lako litakwama, unayemtegemea akusaidie atakuruka na biashara uliyopanga kufanya inaweza kukutia matatani. Mambo yote uliyopanga leo yaache kabisa.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Hii ni siku nzuri hasa Mchana huu kuianza jambo ulilolipanga liwe la kazi au la biashara. Mambop ya mapenzi na usuluhishi hayafai kwa leo. Yaahirishe na upange siku nyingine kuyatatua.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Siku ya leo utageukwa na wale unaowategemea. Pia mambo yako ulyoyapanga nayo yatageuka na kuwa magumu kwako.masuala yako ya biashara yataingia dosari na kuna uwezekano wa kupata hasara.Jaribu kujituliza leo.

NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI TAREHE 8/05/2014:

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Siku ya leo kuna kila dalili kuwa maisha yako yatakuwa mazuri, maradhi au matatizo madogomadogo yatapungua. Vilevile Mkeo au mumeo atakufurahisha kwa zawadi atakayokupa alkhamisi ya leo.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mchana wa leo utapokea habari za kutatanisha kuhusu kazi yako mambo yako ambayo yalikuwa yanakutatiza usiyaguise yanaweza kuleta matata., unashauriwa usianzishe biashara ya aina yeyote kwa wakati huu.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Usipokuwa makini alkhamisi ya leo kuna dalili ya kuwa mambo yako yatafuatiliwa na watu bila ya wewe mwenyewe kujua, kuwa mwangalifu kwa kila hatua utakayoichukua. Kuna mtu unayemuamini sana unatakiwa uwe muangalifu naye anaweza akakudhuru.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo kuna kila ishara ya kukwama kwa mipango yako ya kipesa, mipango ya ndoa au mapenzi itaendelea kama kawaida na kuna mwanamme mrefu mweusi ukikutana naye hiyo itakuwa ni dalili ya kufanikiwa kwa kila jambo.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo kuna dalili kuwa mambo yako hayatakuwa safi na utachukiwa na na kila mtu hapo kazini kwako au mtaani kwenu. Jitahidi kuandaa tafrija na uwakirimu watu ili upate baraka na mikosi ikuondoke.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo kuna kuingiliwa katika kazi zako au kusimamishwa kufanya yale uliyokuwa umeyapanga kuyafanya. Vilevile kuna dalili ya kukimbiwa na Mpenzi wako, unashauriwa kuwa mpole na mwenye subira ili ufanikiwe.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo naona unafikiria mambo ya kushirikiana au kazi na kipato. Ipo dalili kuwa mambo yako kufunguka na mikosi kuonoka. Unashauriwa usijaribu kuingia katika biashara inayoendeshwa na ndugu yako

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Mchana wa leo naona una taabu na magomvi, unalaumiwa na ugonjwa unakutatiza kuna ishara ya kupata mali itakayotokana na urithi au kukabidhiwa mali ya watu uitunze. Lazima katika mambo yako uwashirikishe ndugu zako ndio utafanikiwa.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo kuna dalili yakupata mali au kupewa pesa na watu uliokuwa umewafanyia kazi siku za nyuma lakini walikataa kukulipa. Kuna mpango wa safari uliokuwa unausubiri, mpango huo utafunguka baada ya siku tatu kuanzia leo.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Wiki hii mtoto wako ataugua na kuvuruga mipango yako na utavunjiwa heshima na rafiki yako ambaye hana heshima au wewe utapata maradhi ya kuumwa na kichwa. Kuepusha hayo safiri mbali kwa muda wa wiki.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kwanza ujue kuwa safari ukiwa nayo ni mbaya na mgonjwa yupo ndani ya shida kubwa.Mchana wa leo, hiyo ni dalili ya kwamba hutopata maradhi au kuugua kwa muda mrefu, vile vile ni dalili ya kuletewa zawadi kutoka kwa rafiki yako aliye mbali.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Mchana wa leo hiyo ni dalili kwamba mambo yako mengi yatafanikiwa kwa kuwatumia watu wengine bila ya wewe mwenyewe kushiriki. Tegemea kukutana na mtu mkubwa Serikalini ambaye atakusaidia.

Jumapili, Mei 04, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMATATUTAREHE: 5/5/2014

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Leo upo uwezekano wa kupata mafanikio, huko uendako.hakuna uwezekano wa kutokea matatizo ama iwe kazini kwako au kwa mtu anayekuhusu. ukikutana na mtu kabeba mizigo tegegema kupata fedha

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo hii au wakati wowote ukikutana na Mhubiri, basi itakuwa ni siku nzuri kwa kila jambo utakalolitenda. Unashauriwa kuanzisha mambo mapya leo kwani ndiyo siku yako nzuri.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Wiki hii uhusiano wako na mtu uliyempata hivi karibuni awe ni mpenzi au rafiki utavurugika, Unashauriwa kuwa makini na hao marafiki wapya watakaokujia siku za karibuni.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Wiki hii ikitokea ndugu yako au mpenzi wako aliyekukosea akikuomba radhi au akataka umsamehe, basi hiyo ni dalili kuwa watu wengi wanakukubali kwa kazi zako nzuri unazozifanya, jaribu kuwa karibu na watu wa dini ili kubalikiwa mambo yako.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo hii ukikutana na mtu ambaye hana miguu kabisa, hiyo ni dalili kuibiwa mali yako au kupoteza vitu vya thamani kubwa, vilevile ni ishara ya kukimbiwa na Mkeo au Mpenzi wako au Watoto wako.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Ukikutana na mtu mwenye makovu ya moto Leo hii, hiyo ni dalili kuwa kuna mambo mabaya yanakujia katika biashara au kazi yako, jihadhari na vikundi visivyofaa hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili wakusaidie.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo hii ukikutana mtu mguu wa bandia , hiyo ni ishara kwamba mambo yako yamo hatarini kuharibiwa na watu wakuwa wa serikali au kidini, unatakiwa kuwa mpole kwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 23)
Siku ya leo na wiki hii unashauriwa kutosafiria ili kujikinga na mabalaa katika safari hizo. Jaribu kuwa muangalifu na yoyote utakayeshirikiana naye. Leo hii ukikutana na Mtu anayechechemea, hiyo ni ishara ya kupata matatizo,

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20
Leo hii katika matembezi yako ukikutana na mtu kajipamba Maua, hiyo ni dalili ya kufanikiwa katika mambo yako, unashauriwa kuutumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umeyapanga kuyafanya.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Leo ni siku mbaya kwako kuna uwezekano wa kupata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha. Jaribu kuwa muangalifu mipango yako yote uliyoipanga wiki hii achana nayo.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo hii katika biashara zakoutapata faida ambayo hukuitegemea na yule rafiki yako uliyemkosea utakusamehe madhambi uliyomfanyia. Jitahidi kukutana na wakubwa zako wakusaidie kupata ushauri.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Siku ya leo utapatwa na mambo ya ajabu ajabu, mambo hayo yatakushangaza usijaribu kujibishana na watu usiowajua kunaweza kutokea ugomvi mkubwa.Wiki hii utapata safari ya ardhini itakayokupeleka sehemu ambayo hujawahi kufika.

Jumanne, Aprili 29, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMATANO: 30/4/2014.

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Leo Una woga juu ya mali yako kupotea, au kufukuzwa kazi au kitu chako kupotea. Elewa kwamba adui yako utamshinda na kama una kesi utashinda, ugonjwa unaokusumbua utapona na barua au ujumbe unaotegemea utapata.

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo wale marafiki zako unaowatafuta au kuwahitaji hautakutana nao, Kuna watiu wa mbali ambao watakuletea faraja na mipango mizuri ya kimaisha na kipesa. Shirikiana nao nao na uwakubalie yale wanayotaka utafanikiwa,
.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Mambo yako yapo kizani, umeshajaribu kila njia kupata mwanga lakini imeshindikana na una wasiwasi kuwa utapata matatizo. unashauriwa kuwa muwazi kwa kila jambo unalotaka kulifanya, usiri wowote unaweza kukusababishia hasara ambayo hukuitegemea.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Kuna dalili ya mapenzi kuongezeka kutoka kwa mpenzi wako aliyekuwa akikusumbua, kuna watu watakujia nyakati za asubuhi wakati wowote leo kutaka kufanya na wewe mipango ya kifedha, kubali, lakini kuwa mwangalifu, Unashauriwa kutotoka kwa matembezi nyakati hizo.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Wewe si mtembeleaji wa wenzio, na tabia hiyo inakuletea mikosi na bahati mbaya kwa sababu unapowatembelea unapata bahati fulani. Unashauriwa toka nenda kawatembelee ndugu zako au rafiki zako au wagonjwa kuwa ili kuvuta bahati yako.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo Kuna wanawake watakujia kutaka msaada. Jitayarishe kuwapokea na uwasaidie, kwa kufanya hivyo utajifungulia milango yako ya kimaisha. Kuna wasiwasi wa kukimbiwa na mpenzi wako au rafiki yako unayemuamini kwa kila kitu.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo usimtembelee mtu mtu yoyote, ni wiki mbaya kwako kukutana na watu na ukiwatembelea au kuwashauri mambo yako yatakwama, hasa kama ulikuwa unawategemea watu hao kukufanyia hayo mambo yako.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Jaribu kuwa mpole kwa kila jambo utakalolifanya au litakalokutokea, kwani ubishi kidogo na mabishano yasiyokuwa na msingi ambayo unayapenda yatakuletea matatizo au yatakusababishia kesi kubwa au kipigo.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo kuna ishara kwamba uhusiano wako wa karibu uliokuwa nao kati yako na mpenzi wako utaimarika. Jiepushe na maneno ya kuambiwa. Jaribu kuwadhibiti rafiki zako na wa mpenzi wako wasiwe karibu naye ili kuepusha umbeya.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Hivi sasa unafikiria sana kuhusu taabu mashaka au Matatizo yaliyopo kwa upande wa Mkeo au mumeo au mchumba wako au watu unaoshirikiana nao. Kuna habari utaletewa ya ugonjwa au Mgonjwa, makelele, Ugomvi na taabu ya wazee wako au wakubwa fulani katika Serikali au Kazi.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Muda huu mawazo yako ni namna utakavyowasilisha taarifa zako ofisini. Una hamu ya kujua ni jinsi gani ya kutoa msaada kwa hao waliokuomba uwasaidie. Hapo ulipo una mipango ya kupata pesa na unafikiria jinsi mipango hiyo itakavyokamilika. Mambo yako yatakuwa kama unavyotaka

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Mwezi utakaoanza kesho utasumbuliwa na maradhi ya wasiwasi na yatakusumbua sana. Kubwa zaidi inaonekana una mgogoro mzito na Wazee wako, mkeo, mwanawake wako, mumeo au mwanaume wako.tafuta wazee mpate suluhu au utaharibikiwa.

Jumatatu, Aprili 28, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMANNE ; 30/4/2014

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Wiki hii kuna dalili ya kuwa utafanikiwa katika masuala yako ya kimapenzi au urafiki, kuhusu masuala ya pesa si wakati muafaka kwako. Jaribu kukutana na washirika wako wakusidie katika kupanga mikakati.
 MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo usjishughulishe na kazi yeyote, kuna kila dalili ya kuwa huko uendako hutapata msaada wowote na kama unafuata pesa basi ujue hutapata kitu na kama unafuata ushauri basi ushauri huo utakuwa mbaya na utakupoteza.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Wiki hii kuna uwezekano kwamba utapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wafanyakazi wenzio, Jaribu kuwa mkali na kila hali itakayojitokeza hapo kazini na nyumbani kwako vinginevyo utakumbwa na kashfa mbaya.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Wiki hii ile Mipango yako ya kikazi yako itaendelea kukwama, na kazi uliyoahidiwa na jamaa yako hutaipata, ile hali ya ugonjwa hapo nyumbani kwako haitakwisha. Pendelea kutembelea watoto Yatima na utoe sadaka kuondoa mikosi inayokuandama.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kabla ya wiki hii kumalizika utapata habari mbaya za huzuni au ugonjwa kumfika mtu ambaye unamtegemea sana. Habari hizo zitakutingisha kidogo Jaribu kuwa jasiri ili kukabiliana na hali hiyo.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Wiki hii ni nzuri na huko uendeko ni salama, usiahirishe hiyo safari yako, nenda mapema kabla hayajakukuta makubwa. Makosa uliyoyafanya kwa mpenzi wako hatakusamehe mpaka utafute msuluhishi akusaidie

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo Mawazo yako mengi ni juu ya familia yako, na kupata haja zako au jambo lako ambalo una mategemeo nalo. Una hamu sana ya kukutana na mpenzi wako. Yote unayofikiria yatakuwa baada ya muda wa wiki moja, usiwe na khofu

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Siku ya leo kuna mkutano unaofikiria kama utakuwepo au la na kama upo uhudhurie au usihudhurie. Jua kwamba hivi sasa utapata habari ya sherehe yoyote.na kama ukiitwa kwenye mkutano huo nenda kuna faida.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo Mawazo yako ni juu ya Ndugu Mume au Mke. Kuna upinzani mkali unaokabiliana nao au kuna kesi inayokusumbua au ugonjwa kuumwa wewe au kuuguza.yoyte unayoyafikiria yatakuwa magumu vuta subira

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Leo jioni utakutana macho kwa macho na adui yako au mpinzani wako. Na hiyo ni dalili ya kupata habari nzuri zinazohusiana na mtu ambaye unampenda sana.Leo ni siku nzuri ya kufanya biashara zako

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MARCH 20)
Yule ambaye unamuhisi ni mbaya kwako basi ni mzuri. Shirikiana naye na atakusaidia Tegemea kupata marafiki wengi wapya wiki hii . utapokea habari za kukutatanisha wiki ijayo zichunguze kabla ya kuzifanyia kazi.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Siku ya leo kuna matatizo katika mambo yako utakayoyafanya hasa biashara zako za haramu au za wizi . Jihadhari na kukamatwa, ukitaka kufanikiwa na washirikishe ndugu zako.