Jumatatu, Agosti 07, 2017

IGAD WATAKA UCHAGUZI WA AMANI KENYA

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiserikali wa Nchi za Mashariki na Pembe ya Afrika (Igad) imetola wito kwa washika dau wote katika uchaguzi mkuu wa Kenya kuhakikisha kuwa uchaguzi wa leo unafanyika kwa amani na utulivu.
Tewolde Gebremeskel, Mkuu wa Jumuiya ya Igad amewaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kuwa uchaguzi wa amani nchini Kenya utasaidia kuimarisha uusalama katika kanda ya mashariki mwa Afrika. Amesema Igad inataraji kuwa uchaguzi mkuu unaofanyika leo nchini Kenya utakuwa wa amani kwa sababu Wakenya wameshapata funzo na ibra huko nyuma kwamba machafuko yanaharibu na kutokomeza maendeleo yaliyopatikana kwa miaka mingi. Timu ya waangalizi kutoka Jumuiya ya Igad inatazamia kuwasilisha ripoti yake kuhusu uchaguzu mkuu wa Kenya kesho kutwa Alhamisi. Jumuiya hiyo inaundwa na nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda.

0 comments:

Chapisha Maoni