Alhamisi, Mei 11, 2017

TEKNOLOJIA MPYA KUWEZESHA WATU KUKUSANYA MAJI TOKA HEWANI

Utafiti uliotolewa hivi karibuni kwenye gazeti la Sayansi la Marekani unaonesha kuwa watu wanatazamiwa kukusanya maji kutoka hewani kwa chombo cha kisasa.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Massachusetts na tawi la Berkeley la Chuo Kikuu cha California wamesanifu chombo kinachoweza kukusanya lita kadhaa za maji kutoka kwenye hewa kavu kila siku kwa kutumia nishati ya jua tu.
Mtafiti mmoja kutoka Chuo Kikuu cha California amesema wamepata mafanikio makubwa katika kutatua tatizo la kukusanya maji kutoka hewa kwenye kavu, na hivi sasa hakuna njia nyingine ya kutimiza lengo hilo kwa kutumia nishati ya jua tu. Ingawa chombo cha kuondoa unyevu nyumbani kinaweza kukusanya maji kutoka hewani, lakini kinahitaji umeme mwingi.
Kikundi cha watafiti wa Chuo Kikuu cha California kimesanifu rasilimali yenye mashimo mengi kwa metali ya Zirconium na asidi ya Adipic, na kikundi cha watafiti cha Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Massachusetts walitengeneza chombo cha kukusanya maji kwa kutumia rasilimali hiyo, paneli ya nishati ya jua na ubao wa kupunguza joto.
Watafiti wamesema katika hewa yenye asilimia 20 hadi 30 ya unyevu, kilo moja ya rasilimali hiyo inaweza kukusanya lita 2.8 ya maji kwa nusu siku.
Mtafiti mmoja amesema matumaini yao ni kwamba watu watapata maji jangwani kwa kutegemea chombo hiki

0 comments:

Chapisha Maoni